• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (June 29-July 5)

    (GMT+08:00) 2019-07-05 18:59:17

    Hong Kong yaendelea kulaani vitendo vya kimabavu dhidi ya jengo la bunge

    Jamii ya Hong Kong imeendelea kulaani vitendo vya kimabavu vilivyotokea tarehe mosi katika jengo la bunge, na kutoa wito wa kuhimiza mshikamano, kuanzisha upya mazingira ya kisheria, kuzingatia maendeleo ya uchumi na maisha ya watu, na kulinda ustawi na utulivu wa Hong Kong kwa pamoja.

    Gazeti la Dagong limetoa tahariri ikisema, vitendo vya kimabavu vilivyotokea tarehe mosi vimeonesha wazi kuwa, heshima ya sheria ya sehemu hiyo imevunjwa, na wakitaka kurejesha utaratibu wa kijamii na kulinda maslahi yao ya kimsingi, ni lazima waunge mkono serikali na polisi.

    Shirikisho la Kulinda Haki la Hong Kong limetoa taarifa likihimiza serikali ya Hong Kong kuadhibu vitendo hivyo kwa kufuata sheria, na kuwataka watu wa Hong Kong washikamane, na kukataa vitendo vya kimabavu.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako