• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 14-Septemba 20)

  (GMT+08:00) 2019-09-20 18:23:34
  Kuuawa kwa kiongozi wa FDLR, ishara tosha ya uhusiano mzuri kati ya Kigali na Kinshasa

  Jeshi la DRC lilitangaza siku mbili zilizopita kwamba lilimuua Sylvestre Mudacumura, kiongozi mkuu wa kijeshi kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR), ambalo kwa kipindi cha miongo miwili limeendelea kuhatarisha usalama mashariki mwa DRC.

  Taarifa ya kifo cha Sylvestre MUdacumura, imekaribishwa na serikali ya Kigali. Mauaji ya kiongozi huyo wa kundi la waasi la FDLR ni ishara tosha ya kurejea kwa uhusiano mzuri kati ya nchi hizi mbili jirani, ambazo awali zilikuwa katika uhasama mkubwa, na kusababisha mapigano ya mara kwa mara kwenye mipaka yao.

  Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulikuwa mara zote ukilegalega. Kigali ilivamia DRC mara mbili katika miongo kadhaa iliyopita na ilishtumiwa kusaidia makundi ya waasi kutoka DRC na makundi mengine yenye silaha.

  Kwa upande wa serikali ya Kigali, imesema DRC kuanzia kwa utawala wa Joseph Mobutu hadi utawala wa Joseph Kabila, kwa muda mrefu, ilikuwa mshirika wa karibu wa maadui wake wa FDLR, waasi wa Kihutu, wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya jamii ya Watutsi wa Rwanda mnamo mwaka 1994.

  Uhusiano ulianza kuboreka katika miaka ya hivi karibuni katika utawala wa Joseph Kabila. Uhusiano kati ya nchi hizi mbili umeimarishwa zaidi tangu Felix Tshisekedi kuchukua madaraka ya uongozi wa nchi.

  Kama ishara ya uhusiano mzuri kati ya DRC na Rwanda, Rais wa Rwanda Paul Kagame alizuru Kinshasa mara kadhaa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, na Rais wa DRC Felix Tshisekedi amekuwa akionyesha heshima kwa rais Paul Kagame na kuzuru Kigali.

  Shambulio dhidi ya Sylvestre Mudacumura na maafisa wake ni ishara tosha ya hivi karibuni ya Kinshasa kwa serikali ya Kigali, kwani serikali ya DRC imekuwa ikionyesha ishara nzuri kwa jirani yake katika miezi ya hivi karibuni ikiwa ni wakati muhimu katika historia yake.

  Pamoja na kurudishwa kwa nguvu kwa mamia ya waasi wa FDLR na familia zao, Kinshasa pia ilikabidhi Kigali msemaji wa kundi la FDLR, La Forge Fils Bazeye, mwanzoni mwa mwaka huu.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako