• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 14-Septemba 20)

    (GMT+08:00) 2019-09-20 18:23:34

    Ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya China yalaani uingiliaji wa Marekani katika mambo ya Hong Kong

    Ofisi ya wizara ya mambo ya nje ya China katika mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong (HKSAR) imelaani spika wa bunge la Marekani kwa kuwaunga mkono wafarakanishaji wa Hong Kong.

    Msemaji wa ofisi hiyo amesema spika huyo Bibi Nancy Pelosi amemkaribisha mfarakanishaji Bw. Joshua Wong kwenye ofisi za bunge na kuingilia mambo ya ndani ya China kwa kisingizio cha kutimiza uhuru na haki. Amesema kitendo chake kimekwenda kinyume na msimamo wa Marekani wa kuunga mkono sera ya "nchi Moja, Mifumo Miwili" na kuonesha hila yao ya kisiasa inayojificha.

    Msemaji huyo pia amesema uhuru na haki ya watu wa Hong Kong ni kusimamisha vurugu na kurejesha utaratibu. Amehimiza baadhi ya wanasiasa wa Marekani kuacha kiburi na ubaguzi, kuheshimu nia ya watu wengi wa Hong Kong na kuacha kuingilia mambo ya ndani ya Hong Kong, China.

    Wachambuzi wanasema kitendo hicho cha Bibi Pelosi kinalenga kuwaunga mkono viongozi wa wafarakanishaji mkoani Hong Kong na kutafuta "wakala" wa Marekani kama inavyofanya "mapinduzi ya rangi" katika sehemu nyingine duniani. Mambo yanayotokea mkoani Hong Kong katika siku za hivi karibuni yameonyesha kuwa dhana za "haki za binadamu" na "uhuru" zimepotoshwa na kutumiwa vibaya, na kuwa visingizio vya baadhi ya watu wa Hong Kong wanaosahau mababu zao kuvuruga Hong Kong na kufanya matembezi hapa na pale, na vya baadhi ya watu wa magharibi wanaoipinga China kuharibu mstari wa mwisho wa "Nchi Moja, Mifumo Miwili".


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako