• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 14-Septemba 20)

  (GMT+08:00) 2019-09-20 18:23:34

  Rais wa zamani wa Tunisia Zine el-Abidine Ben Ali aaga dunia

  Rais wa zamani wa Tunisia Zine el-Abidine Ben Ali amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83, wakili wake amesema.

  Baada ya mihula mitano katika uongozi wa nchi, Ben Ali alilazimika kuondoka madarakani kufuatia kuzuka kwa maandamano makubwa.

  Ben Ali alikuwa anaishi uhamishoni nchini Saudi Arabia tangu kuanguka kwa utawala wake mnamo mwaka 2011.

  Tangu mwaka 2011, kiongozi huyo wa zamani alikuwa amekimbilia Jeddah, kwenye mwambao wa Bahari Nyeusi, nchini Saudi Arabia, pamoja na baadhi ya watu wa familia yake, kufuatia maandamano ya raia yaliyozuka katika baadhi ya nchi za Kiarabu.

  Mnamo mwaka 2018, baada ya kesi kadhaa ambazo hakuripoti, Ben Ali alihukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 200 jelakwa mashtaka mbali mbali ikiwa ni pamoja na mauaji, uporaji, ufisadi mateso.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako