• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 14-Septemba 20)

  (GMT+08:00) 2019-09-20 18:23:34

  Iran yasema haitafanya mazungumzo na Marekani kabla ya kuondolewa vikwazo

  Msemaji wa serikali ya Iran Bw. Ali Rabiee amesema nchi hiyo haitafanya mazungumzo na Marekani kabla ya kuondolewa vikwazo.

  Hata hivyo amesema kama rais Donald Trump akipata imani kutoka Iran na kuiheshimu nchi hiyo, wataweza kujadiliana kwenye utaratibu wa kundi la nchi tano wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani.

  Wakati huohuo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bw. Abbas Mousavi amesema kwa mujibu wa mpango wa sasa, rais Hassan Rouhani hatakutana na rais Donald kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa unaofanyika mjini New York. Bw. Mousavi amesisitiza kuwa mkutano sio kwa ajili ya picha, bali ni kufikia matokeo halisi.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako