• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 21-Septemba 27)

  (GMT+08:00) 2019-09-27 18:23:41

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi wiki hii mjini New York amehudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kuhusu suala la nyuklia la Iran.

  Bw. Wang Yi amesema, Marekani kutoa shinikizo kubwa dhidi ya Iran ni chanzo cha kimsingi cha msukosuko wa suala la nyuklia la Iran. Kama hali hiyo itazidi kuwa mbaya, itasababisha msukosuko mkubwa zaidi, na kuzitaka pande mbalimbali zifanye juhudi kuhimiza suala la nyuklia la Iran litatuliwe kwa njia ya kisiasa na kidiplomasia.

  Amesema China ina mapendekezo manne kuhusu suala hilo, ikiwemo kushikilia kanuni ya kimsingi ya kulinda utaratibu wa pande nyingi, kushikilia kutekeleza ahadi ya makubaliano, kushikilia njia sahihi ya kutatua migongano kwa njia ya mazungumzo, na kushikilia mwelekeo wa kuhimiza amani ya kikanda.

  Bw. Wang Yi pia amehudhuria mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na mashirika ya kikanda kuhusu ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi.

  Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi wiki hii amekutana na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahammat kando ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

  Bw. Wang Yi amesema, kwa sasa uhusiano kati ya China na Umoja wa Afrika uko katika kipindi kizuri kihistoria, matokeo mbalimbali ya ushirikiano yanatekelezwa, na China inapenda kushirikiana na Afrika, kuimarisha ushirikiano katika amani na usalama, afya ya umma, maendeleo na sekta nyingine. Amesema China inatumai Umoja wa Afrika unaweza kuchukua nafasi yake katika kuendeleza uhusiano kati ya Afrika na China.

  Kwa upande wake Bw. Faki amepongeza maadhimisho ya miaka 70 tangu Jamhuri ya watu wa China ianzishwe. Amesema, mafanikio yaliyopatikana na China katika miaka 70 iliyopita ni ya kipekee duniani, na yanatokana na uongozi hodari wa China na juhudi za wananchi wake. Ameongeza kuwa, Umoja wa Afrika unatarajia kuimarisha ushirikiano na China, kulinda kwa pamoja hali ya pande nyingi na kulinda hadhi na umuhimu wa Umoja wa Mataifa.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako