• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 21-Septemba 27)

  (GMT+08:00) 2019-09-27 18:23:41

  Boris Johnson akosolewa na Mahakama ya Juu

  Wabunge nchini Uingereza wamerejea bungeni wiki hii, baada ya Mahakama ya Juu kuamua kuwa hatua ya Waziri Mkuu Boris Johnson kusitisha bunge kwa wiki tano, ilikuwa kinyume cha sheria.

  Waziri Mkuu Boris amelazimika kuondoka mapema kwenye Mkutano Mkuu wa umoja wa Mataifa jijini New York, kuwakabili wabunge wa upinzani.

  Boris hata hivyo amesema hakubaliani na uamuzi huo wa Mahakama.

  Akisoma uamuzi huo, jaji mkuu wa mahakama ya juu ya Uingereza Brenda Hale, amesema majaji wa mahakama hiyo wamefikia uamuzi huo kwa pamoja, na kuongeza kuwa uamuzi wa Johnson kuahirisha bunge haukuwa halali.

  Hata hivyo Boris Johnson amegoma kujiuzulu baada ya pigo hilo la mahakama ya juu.

  Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya uamuzi huo wa mahakama mjini London, Boris Johnson ambaye alikuwa mjini New York akihudhuria Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa, amepuuza miito iliyotolewa na wanasiasa mbali mbali wakimtaka ajiuzulu, akisema kuwa kwa maoni yake, uamuzi wa mahakama ya juu haukuwa sahihi.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako