• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 21-Septemba 27)

    (GMT+08:00) 2019-09-27 18:23:41

    Mkutano wa kilele wa malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa wapitisha azimio la kisiasa

    Mkutano wa kilele wa malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa umefanyika huko New York na kupitisha azimio la kisiasa, ambalo nchi wanachama wa umoja huo zimeahidi kuchangisha fedha ndani ya miaka 10 ijayo ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu kabla ya mwaka 2030.

    Mwenyekiti wa baraza kuu la 74 la Umoja wa Mataifa Bw. Tijjani Muhammad-Bande akihutubia ufunguzi wa mkutano huo alisema, kuhimiza utaratibu wa dunia ya ncha nyingi ni chaguo pekee linaloweza kukabiliana na changamoto za dunia.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema kwenye njia ya kutimiza malengo hayo, bado hakuna shahaba na kuna vizuizi vipya hivi sasa, ikiwa ni pamoja na mapambano yanayosababisha vifo, mgogoro wa halitabia, ukatili wa kijinsia, uwiano mbaya wa ukuaji wa kiuchumi, kuongezeka kwa kiwango cha madeni, hali ya wasiwasi ya biashara ya dunia na nyinginezo. Hatua husika lazima zichukuliwe ili kuziunga mkono nchi zinazoendelea katika mageuzi yao ya kisiasa na kiuchumi.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako