• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 21-Septemba 27)

  (GMT+08:00) 2019-09-27 18:23:41

  Nancy Pelosi atangaza kuanza uchunguzi dhidi ya Donald Trump

  Spika wa Baraza la Wawakilishi kutoka chama cha Democratic nchini Marekani Nancy Pelosi ametangaza kwamba uchunguzi kwa mashtaka dhidi ya Donald Trump umeanza rasmi.

  Rais huyo wa Marekani anatuhumiwa kuwa alimuomba mwenzake wa Ukraine kumchunguza mpinzani wake wa kisiasa Joe Biden kwa madai ya ufisadi.

  Wabunge wa Chama cha Democratic wamesema kuwa Trump alijaribu kuitisha nchi Ukraine kuwa hataitolea msaada wa kijeshi iwapo haitamchunguza Biden.

  Spika wa bunge ambaye pia ni kiongozi wa juu wa cham cha Democratic Nancy Pelosi, amesema rais Trump ni lazima awajibike.

  Hii ni hatua ya kwanza katika mashtaka ya kumng'atua madarakani rais wa Marekani, ambaye Baraza la Wawakilishi linamshutumu kwa kufanya matumizi mabaya ya madaraka.

  Baraza la Wawakilishi litachunguza ikiwa Donald Trump alitafuta msaada kutoka Ukraine ili kupata taarifa inayoweza kumuweka matatani Joe Biden, ambaye anapewa nafasi kubwa katika kinyang'anyiro cha kumteuwa mgombea kutoka chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 nchini Marekani.

  Rais Trump hata hvyo, kwenye ukurasa wake wa Twitter, amepuuzilia mbali harakati za wabunge wa Democratic na kusema hatua hiyo itamsaidia kushinda Uchaguzi mwaka ujao.

  Utaratibu wa kumg'oa rais madarakani unafanyika kwa hatua kadhaa. Baraza la Wawakilishi linachunguza na, ikiwa ni lazima, linaandika na kupiga kura kwa wingi wa sauti kuhusu kumfungulia mashitaka rais. Ikiwa Baraza la wawakilishi litapiga kura ya kumg'oa rais madarakani, hatua inayofuata ni Bunge la Seneti kuanda kesi. Uamuzi wa kumuweka rais hatiani hupitishwa na iwingi wa theluthi mbili.

  Joe Biden ni miongon mwa viongozi wa juu wa chama cha Democratic ambao wametangaza kuwania urais nchini Marekani.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako