• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi na biashara 11-12-2019

    (GMT+08:00) 2019-12-11 20:18:08

    Tanzania: Kilimo ndicho kitaisaidia taifa la Tanzania katika ukuaji wake wa uchumi. Haya ni kulingana na Benki ya Dunia ambayo imesisitiza kwamba kilimo kikitiliwa maanani, basi kitashinda sekta zingine zote katika kuiletea tija kiuchumi taifa zima la Tanzania. Hata hivyo, Benki ya dunia inasema kwamba lazima serikali ya Tanzania ihakikishe kuwa inarekebisha sera na masharti mengine yaliyopo kwa sasa, katika sekta ya kilimo.

    Kwenye toleo lake la 13 linalohusu ripoti ya uchumi nchini Tanzania, kwa jina Transforming Agriculture, Benki ya Dunia inasema kwamba kilimo kimetoa ajira kwa zaidi ya watanzania asilimia 67, na inachangia takriban asilimia 30 ya pato zima la taifa.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako