• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi na biashara 11-12-2019

    (GMT+08:00) 2019-12-11 20:18:08

    Rwanda: Kuna shinikizo kwa serikali ya Rwanda kutoka kwa watetezi wa haki za binadamu, kwamba waajiri wote nchini Rwanda watenge asilimia tano ya nafasi za ajira kwa watu wanaoishi na ulemavu.

    Kulingana na watetezi wa haki za binadamu, hatua hii itasaidia sana kupunguza ukosefu wa ajira kwa Warwabda wanaoishi na hali ya ulemavu. Vile vile, lipo shinikizo kwa serikali kuwapa walemavu mafunzo ya ujuzi mbali mbali ili waweze kujikimu kimaisha.

    Kulingana na Emmanuel Ndayisaba, ambaye ni katibu mkuu wa NCPD, endapo kutakuwa na ushirikiano kutoka sekta mbali mbali kuhusiana na swala hili, basi zaidi ya nafasi 2000 za ajira zitapatikana ifikapo mwaka wa 2020. Nafasi hizi hazitakuwa za ajira ya shambani.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako