• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Decemba 21-Decemba 27)

    (GMT+08:00) 2019-12-27 20:13:06

    Wanawake 31 wauawa kwenye shambulio la waasi Burkinafaso

    Watu 35 wameuawa katika shambulio lililolenga kambi moja ya kijeshi na mji mkuu wa Burikina Faso nchini humo.

    Maofisa wa serikali wanasema wanajeshi saba na wapiganaji 80 waliuawa baada ya jeshi kukabiliana na shambulio hilo la Jumanne katika mkoa wa Arbinda uliopo kaskazini mwa Soum.

    Rais Roch Marc Christian Kabore alitangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika.

    Hadi wakati wa kwenda hewani hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza shambulio hilo. Nchi hiyo ambayo imekuwa na amani imekumbwa na ghasia za kiwango cha juu kufuatia uvamizi wa mara kwa mara mbali na kusambaa kwa wapiganaji nchini Mali .

    Mamia ya watu wameuawa mwaka huu huku mamilioni kati yao wakiwachwa bila makao.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako