• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Decemba 21-Decemba 27)

    (GMT+08:00) 2019-12-27 20:13:06
     

    Uturuki kutuma vikosi vya jeshi nchini Libya

    Uturuki imesema serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa nchini Libya imeiomba nchi yake kupeleka vikosi vya jeshi kuulinda mji mkuu wa Tripoli dhidi ya mashambulizi ya vikosi hasimu. Erdogan amesema bunge la Uturuki litajadili na kupiga kura katika muda wa hadi wiki moja kuamua kuhusu ombi hilo na kuongeza serikali yake itawasilisha muswada wa kupeleka vikosi Uturuki nchini Libya.

    Akizungumza na maafisa wa chama tawala, rais wan chi hiyo Reccip Tayyip Erdogan amesema serikali ya mjini Tripoli inayoongozwa na waziri mkuu Fayez Sarraj imeikaribisha Uturuki kutuma vikosi vyake chini ya makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi yaliyotiwa saini hivi karibuni na pande hizo mbili.

    Uturuki na Libya pia zilitiliana saini mkataba kuhusu eneo la bahari ya Mediterrania ambayo yote pamoja na ule wa ushrikiano wa kijeshi ilikabiliwa na ukosoaji kutoka kanda hiyo na pande nyingine za ulimwengu. Utawala wa waziri mkuu Sarraj umekabiliwa na uchokozi tangu mnamo mwezi April kutoka serikali hasimu ya upande wa mashariki na vikosi vinavyoongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar, ambaye anajaribu kuchukua udhibiti wa mji mkuu, Tripoli.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako