• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Decemba 21-Decemba 27)

  (GMT+08:00) 2019-12-27 20:13:06

  Misri, Sudan na Ethiopia kutatua tofauti zao juu yam to Nile

  Serikali ya Misri imesema kwamba Misri, Ethiopia na Sudan zinakaribia kutatua tofauti zao juu ya utumiaji na usimamizi wa bwawa la kuzalisha umeme linalojengwa na Ethiopia.

  Tangazo hilo limetolewa baada ya mawaziri wa nchi hizo tatu kukutana mjini Khartoum mwishoni mwa wiki.

  Misri ilikuwa na wasiwasi kwamba mradi wa Grand Ethiopia Renaissance Dam, GERD, unaojengwa wakati huu karibu na mpaka kati ya Ethiopia na Sudan, kwenye mto wa Blue Nile, utapunguza maji ambayo tayari yamepungua sana katika mto Nile inayotegemea sana.

  Waziri wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Sudan Yasser Abbas amesema kwa muda wa miezi kadhaa hivi karibuni nchi hizo tatu zimekuwa zikikutana kujaribu kufikia makubaliano juu ya matumizi ya bwawa hilo. Mwezi Novemba mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Ethopia, Misri na Sudan walikubaliana kufanya kazi pamoja kutanzua ugomvi wao juu ya bwawa litakalo gharimu dola bilioni 4 ifikapo Januari 15, 2020


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako