• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Decemba 28-Januari 3)

    (GMT+08:00) 2020-01-03 18:37:17

    Lakini je, nini kilichofanyika?

    Ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinasema kuwa Jenerali Soleimani na maafisa wa waasi wanaoungwa mkono na Iran nwalikuwa wakiondoka katika uwanja wa ndege wa Baghdad kwa kutumia magari mawili wakati waliposhambuliwa na ndege za Marekani zisizokuwa na rubani karibu na eneo la kuweka mizigo.

    Kamanda huyo aliripotiwa kusafiri kutoka Lebanon au Syria. makombora kadhaa yaliripotiwa kushambulia msafara wao, ambapo karibu watu watano wanaaminiwa kuawa.

    Taarifa iliyotolewa na Pentagon ilisema: "Kufuatia agizo la rais, vikosi vya jeshi la Marekani vilichukua hatua ya kuwalinda wafanyikazi wake nje ya nchi kwa kumuua Qasem Soleimani,"

    "Hatua hii ililenga kudhibiti mipango ya Iran ya mashabulio ya siku zijazo. Marekani itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuwalinda watu wetu na maslahi yetu kote duniani," ripoti hiyo iliendelea kusema.

    Shambulio hilo la ndege zisizo na rubani linakuja baada ya siku kadhaa za maandamano ambapo waandamaanaji waliokuwa wakishambulia ubalozi wa Marekani mjini Baghdad kukabiliana na vikosi vya Marekani katika eneo hilo.

    Pentagon inasema jenerali Soleimani aliidhinisha mashambulio dhidi ya ubalozi wa Marekani.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako