• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Decemba 28-Januari 3)

  (GMT+08:00) 2020-01-03 18:37:17

  Mahakama yamnyima kibali Kabendera kwenda kushiriki mazishi ya mama yake

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemnyima kibali mwandishi wa habari, Erick Kabendera, kwenda kushiriki ibada ya maziko ya mama yake mzazi, Verdiana Mujwahuzi. Janeth Mtega amesema Mahakama ya Kisutu haina Mamlaka ya kumruhusu Kabendera kuhudhuria mazishi ya Mama yake, hivyo atarudi Mahabusu hadi tarehe itakayopangwa na hakuna fursa ya kukata rufaa katika maamuzi hayo, Kesi imeahirishwa hadi January 13, 2020.

  Hapo awali baada ya wakili wa Kabendera kuomba ruhusa hiyo, Wakili Wankyo alidai kuwa maombi ya Kabendera kupitia mawakili wake yamewasilishwa wakati ambao si sahihi kwa sababu mahakama haina mamlaka na pia Mkurugenzi wa Mashtaka hajaipa kibali ya kusikiliza kesi hiyo.

  Kukataliwa kwa Kabendera kushiriki mazishi ya mama yake, kumeibuka kutokana na maombi aliyoyatoa Kabendera kupitia mawakili wake akiwemo Jebra Kambole.

  Mama Kabendera alifariki dunia Desemba 31, 2019, ikiwa ni wiki kadhaa baada ya kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amsamehe mwanaye huyo,.

  Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh.Mil 173.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako