• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 15-February 21)

    (GMT+08:00) 2020-02-21 19:13:25

    Waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane kushtakiwa kwa mauaji ya mkewe.

    Waziri Mkuu wa Lesotho Thomas Thabane, 80, atashtakiwa kwa mauaji ya mkewe wa kwanza Lipolelo Thabane, Polisi wameeleza. Bwana Thabane alitangaza kuwa atajiuzulu mwezi Julai kutokana na umri wake, bila kuzungumzia shutuma dhidi yake.

    Mkewe wa sasa Maesaiah Thabane tayari ameshtakiwa kwa mauaji.

    Atakuwa kiongozi wa kwanza kusini mwa Afrika kushtakiwa kwa mauaji akiwa madarakani, katika kesi ambayo imeishitua nchi hiyo.

    Lipelo 58, alipigwa risasi na kufa siku mbili kabla bwana Thabane kuwa waziri mkuu mwaka 2017.

    Wakati huo, alieleza kuwa kitendo cha mauaji ya mkewe wa zamani ''hakina maana'' lakini sasa polisi wanamshutumu kuhusika kwenye mauaji hayo.

    Mkewe wa zamani Lipoleo Thabane alipigwa risasi na kufariki nje ya nyumba yake katika mji mkuu wa Maseru siku mbili kabla ya kuapishwa kuwa waziri mkuu 2017.

    Wanandoa hao walikuwa wakikabiliwa na mchakato wa kutalakiana.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako