• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 15-February 21)

    (GMT+08:00) 2020-02-21 19:13:25

    Watoto wafariki kwa kula vitafunwa vilivyopikwa kwa dawa ya kuulia wadudu

    Watoto wawili nchini Uganda wamefariki dunia huku wengine 11 wakipelekwa hospitali baada ya kula kitafunwa mfano wa hamri maarufu kama, Kabalagala kilichotengenezwa kwa sumu ya kuuwa wadudu badala ya mafuta, gazeti la Daily Monitor newspaper linaripoti.

    Watoto wote 13 wanatoka familia moja Budumba, magharibi mwa Uganda na kusemekana kwamba walikuwa na umri wa 5 na 6. Gazeti hilo limeripoti kwamba watoto hao walijipikia wenyewe vitafunwa hivyo mfano wa mahamri ambavyo vinafahamika kama Kabalagala.

    Watoto hao inasemekana kwamba miongoni mwa viambato walivyotumia wakati wanapika ilikuwa dawa ya kuua wadudu inayonyunyizwa kwenye matikiti maji na mbogamboga zinazokuzwa wakidhani kwamba ni mafuta.

    Kulingana na gazeti hilo, watoto hao walianza kutapika na kupelekwa hospitali ya Busolwe ambapo wawili wao waliaga dunia huku wengine 11 wakiendelea kupata matibabu. Akithiitisha kisa hicho, mkuu wa polisi wa eneo Ceasar Tusingwire alithibitisha tukio hilo.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako