• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 15-February 21)

    (GMT+08:00) 2020-02-21 19:13:25

    Maisha ya baadae ya watoto wa sasa yamo hatarini. Yasema WHO.

    Hakuna nchi inayotoa fursa ya malezi ya kiafya na mazingira yanayofaa kwa ajili ya hali zao za baadae, linasema Shirika la afya Duniani (WHO).

    Wataalamu wanasema mabadiliko ya hali ya hewa na matangazo ya kudhuru yanayoshawishi ulaji wa vyakula vinavyopatikana kwa urahisi na unywaji wa pombe wa watoto wadogo vinawaweka watoto katika hatari.

    Uingereza iliwekwa katika nafasi ya 10 miongoni mwa nchi zenye afya na hali bora ya maisha ya watoto.

    Hata hivyo iliashindwa katika kuyalinda mazingira ya siku za usoni ya watoto .

    Ripoti ya shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef na tume ya Lancet zilitaja nchi 180 katika uwezekano wa watoto kuweza kuishi vizuri, kwa kuzingatia afya na maisha bora ya watoto kama vile kuwapatia elimu, vyakura vyenye virutubisho na kiwango cha vifo vya watoto.

    Nchi hizo pia ziliwekwa katika viwango kwa kuzingatia uwezo wao wa utoaji wa hewa ya kaboni.

    Wataalamu takriban 40 wa afya ya watoto walionya kuwa miongo miwili ijayo "itakua ya madhara" ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa na serikali kote duniani.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako