• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 29-Machi 6)

    (GMT+08:00) 2020-03-06 20:06:50

    China yaahidi kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na maambukizi ya COVID-19 duniani

    Tangu mlipuko wa virusi vipya vya korona COVID-19 utokee, China imesimama katika mstari wa mbele kupambana nao, huku ikishirikiana na jamii ya kimataifa na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya ulinzi wa afya ya umma duniani. Katika mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa leo hapa Beijing, maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China na Kamati ya Afya ya China wameahidi kuwa China itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kuzuia kuenea kwa virusi duniani na kujenga kwa pamoja jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Maambukizi ya COVID-19 ni tishio na changamoto kubwa kwa maisha na afya ya watu wa China, na wa dunia nzima. Katika mapambano dhidi na COVID-19, China siku zote imefuata wazo la jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, kusimama kithabiti katika mstari wa mbele wa mapambano hayo, ikishirikiana na jamii ya kimataifa. Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Ma Zhaoxu anasema,

    "Serikali ya China imekuwa ikitoa taarifa kuhusiana na maambukizi hayo kwa wakati na kufuata kanuni ya uwazi na uwajibikaji, kujitahidi kujibu ufuatiliaji wa pande mbalimbali na kuimarisha ushirikiano na jamii ya kimataifa. Tumetoa taarifa mbalimbali kwa Shirika la Afya Duniani WHO kwa wakati kuhusiana na ugonjwa huo, ikiwemo mpangilio wa vinasaba vya virusi. Hatua hizo zimepongezwa sana na jamii ya kimataifa ikiwemo WHO."

    Ma amesisitiza kuwa, China imejitahidi kuzuia kuenea kwa virusi vya COVID-19 duniani, kama alivyosema mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghjebreyesus, hatua madhubuti zinazochukuliwa na China sio tu zinalinda maisha ya wachina, bali pia binadamu wote, na kufanya nchi nyingine duniani ziwe na muda wa kujiandaa.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako