• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 25-Mei 1)

    (GMT+08:00) 2020-05-01 19:54:56

    China na Afrika zashirikiana kwenye mapambano dhidi ya Corona

    Nchi nyingi za Afrika zikiwemo Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Benin na Angola, zimeimarisha hatua zao za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona yanayoenea kwa kasi barani Afrika. China ikiwa ni mwenzi wa nchi za Afrika, imetoa misaada kwa bara hilo kupitia njia mbalimbali.

    Hivi karibuni, wataalamu wa matibabu wa China wametoa uzoefu wao kuhusu kinga na tiba ya Corona kwa njia ya video kwa madakari na maofisa wa wizara za afya katika nchi mbalimbali za Afrika, ikiwa ni pamoja na Kenya, Misri, Morocco, Angola na Madagascar. Wataalamu na maofisa wa nchi hizo wameipongeza China kwa mafanikio iliyopata katika kudhibiti mlipuko wa virusi vya Corona na mchango iliotoa katika kulinda usalama wa afya ya umma duniani. Pia wamesisitiza kuwa uzoefu na hatua zilizochukuliwa na China ni mfano wa kuigwa kwa nchi za Afrika katika kudhibiti virusi hivyo.

    Mbali na kutoa uzoefu wake, serikali ya China na mashirika ya kiraia pia yametoa misaada ya vifaa vya tiba kwa nchi za Afrika. Maofisa wa nchi za Afrika waliohudhuria halfa za kupokea vifaa hivyo kutoka China, wamesema nchi zao zitatumia vizuri vifaa hivyo, kujifunza uzoefu wa China na kushirikiana na China, ili kuweza kushinda mapema mapambano hayo dhidi ya virusi vya Corona.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako