• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 25-Mei 1)

    (GMT+08:00) 2020-05-01 19:54:56

    China yasema lawama dhidi yake ni kinyume cha hali halisi

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Le Yucheng amesema, mlipuko wa virusi vya Corona sio kosa la China, bali ni maafa ya kiasili kwa nchi zote ikiwemo China.

    Akizungumza katika mahojiano na Kituo cha Habari cha NBC cha Marekani, Bw. Le amesema, China imetoa mchango na kushiriki katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo. Amesema madai ya kuitaka China kuwajibika na mlipuko huo duniani na kulipa fidia ni mchezo wa kisiasa ambalo linajaribu kukwepa kuwajibika kwa kutofanya vizuri katika kupambana na maambukizi ya virusi hivyo.

    Bw. Le pia amesema, katika kipindi hiki muhimu, China na Marekani zinapaswa kuacha tofauti zilizopo na kushirikiana kupambana na adui wa pamoja ambaye ni virusi vya Corona.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako