• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 13-Juni19 )

    (GMT+08:00) 2020-06-19 20:44:11

    Mkutano wa Focac kwa mara ya kwanza wafanywa kwa njia ya video

    Kwa mara ya kwanza mkutano wa Focac umefanyika kwa njia ya video ambapo marais walijadiliana njia mwafaka za kupambana na Covid 19 huku China ikitoa ahadi za kuzisaidia nchi za Afrika katika mapambano dhidi ya virusi hivyo. Ahadi za China zilizotolewa kwenye mkutano huo maalumu wa kilele wa Mshikamano wa China na Afrika dhidi ya COVID-19 zitasaidia Afrika kupata vifaa vya matibabu katika kupambana na virusi vya Corona na kuanza mapema ujenzi wa makao makuu ya Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) utasaidia kuleta pumzi mpya katika mapambano dhidi ya virusi hivyo. Mtaalam wa Ushirikiano wa Kimataifa hasusuan kuhusu uhusiano kati ya China na Afrika Cavince Adhere amepongeza ahadi ya China ya kutoa vifaa zaidi, kupeleka timu za wataalam, na kuanza mapema ujenzi wa makao makuu wa Africa CDC.

    Kwenye mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video rais wa China Xi Jinping alisema China itaanza ujenzi wa makao makuu ya Africa CDC mwaka huu, kabla ya muda uliopangwa, na itaendelea kuzisaidia nchi za Afrika kwa kutoa vifaa, kupeleka timu za wataalam, na kuiwezesha Afrika kununua vifaa vya matibabu kutoka China.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako