• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 13-Juni19 )

    (GMT+08:00) 2020-06-19 20:44:11

    Kenya yapata kiti kwenye baraza la umoja wa mataifa

    Hatimaye Kenya imeshinda nafasi isiyo ya kudumu kwenye baraza la Umoja wa mataifa. Kenya iliishinda Djibouti siku ya Alhamisi kufuatia duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Kenya sasa inakuchua nafasi isiyo ya kudumu kwenye baraza hilo kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia tarehe 1, Januari, mwakani.

    Jumatano mshindi alishindwa kupatikana kati ya nchi hizo mbili, ambazo zilikuwa zimejitosa uwanjani kuwania nafasi hiyo.

    Hatimaye Kenya iliibuka mshindi baada ya kupata theluthi mbili ya kura zote zilizopigwa Alhamisi, kama inavyohitajika na kanuni za baraza hilo.

    Nchi zipatazo 191 zilipiga kura, Kenya ilipata kura 129 huku Djibouti ikizoa kura 62.

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alionyesha fahari yake baada ya kufahamishwa kuhusu ushindi huo, akitaja ushindi huo kuwa unaonyesha imani ambayo jumuiya ya kimataifa inayo kwa nchi yake. Hii itakuwa mara ya pili kwa Kenya kuketi kwenye baraza hilo. Ilikuwa moja ya wawakilishi wa bara la Afrika kati ya mwaka wa 1996 na 1997.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako