• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 13-Juni19 )

    (GMT+08:00) 2020-06-19 20:44:11

    Raia mwengine mweusi wa Marekani afariki mikononi mwa polisi

    Maandamano ya kupinga ubaguzi na matumizi ya nguvu yanayofanywa na polisi, yalipata shinikizo jipya mwishoni mwa wiki hapa Marekani kufuatia kifo cha Mmarekani mwingine mweusi mjini Atlanta, Georgia.

    Tukio hilo limesababisha kuongezeka wito wa kupitishwa sheria kuhusu mageuzi kwenye jeshi la polisi na mfumo wa sheria.

    Maelfu ya watu walijitokeza katika miji kadhaa nchini Marekani na kwengineko duniani kudai mageuzi ya haraka katika jinsi polisi inavyofanyakazi ili kuzuia utumiaji nguvu.

    Maandamano ya mwishoni mwa wiki yaligubikwa na kifo kingine cha Rayshard Brooks aliyepigwa risasi na polisi mzungu alipokataa kukamatwa nje ya mgahawa wa wendys huko Atlanta ijumaa usiku. Kulingana na video iliyotolewa na polisi Brooks mwenye umri wa miaka 27 aliyekuwa amelala ndani ya gari lake karibu na dirisha la mgahawa wa Wendy la kuhudumia wateja, alibainika amelewa na polisi alipotaka kumkamata alikataa na wakaminyana kidogo na Brooks alipokuwa anakimbia afisa wa polisi alimfyetulia risasi.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako