• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 4-Julai 10)

    (GMT+08:00) 2020-07-10 16:09:32

    CORONA YALEMAZA MASOMO KENYA

    Wanafunzi wote wa shule za msingi na upili watalazimika kurudia madarasa mwaka ujao, baada ya serikali kufutilia mbali ratiba ya masomo mwaka huu kutokana na janga la corona.

    Waziri wa Elimu, Prof George Magoha, alitangaza pia kwamba, kutokana na mashauriano baina ya wadau hakutakuwa na mitihani ya Darasa la Nane (KCPE) na Kidato cha Nne (KCSE) mwaka huu.

    Matumaini kwamba shule zingefunguliwa ifikapo Septemba, au angalau watahiniwa kuruhusiwa kurejea shuleni sasa yametokomea kwa kuwa maambukizi ya virusi vya corona yanaendelea kuongezeka, na yanatarajiwa kufika kileleni Septemba.

    Taasisi za elimu ya juu pekee ndizo zitaanza kufunguliwa kwa zamu wakati huo, kwa mujibu wa waziri.

    Akitoa taarifa hiyo siku ya Jumanne wiki hii jijini Nairobi, Prof Magoha alisema maamuzi hayo ya Jopo Maalum la Wataalamu yalimridhisha Rais Uhuru Kenyatta. Wanafunzi waliokuwa wamesajiliwa kufanya mtihani wa KCSE mwaka huu ni 752,836 huku wale waliosajiliwa kufanya mtihani wa KCPE wakiwa milioni 1.2.

    Alieleza kuwa, sababu nyingine ya kuahirisha mitihani ya kitaifa ni kwamba, ingekuwa vigumu kwa wanafunzi walio katika Darasa la Saba na Kidato cha Tatu kukamilisha mihula iliyobaki kwa muda mfupi uliosalia.

    Sababu nyingine ya hatua hiyo ni kuwa, ikiwa wanafunzi wangeruhusiwa kusafiri kurejea katika shule zao kwa kuabiri magari, hilo lingewaweka kwenye hatari ya kuambukizwa na kusambaza virusi hivyo.

    Hatua hii itakuwa pigo kwa walimu wa shule za kibinafsi na wale wanaoajiriwa na bodi za usimamizi wa shule ambao wengi wao hawajapokea mishahara tangu Machi. Wadau wa elimu waliozungumza katika kikao hicho cha wanahabari walieleza kuridhika na hatua hiyo ya serikali.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako