• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 4-Julai 10)

    (GMT+08:00) 2020-07-10 16:09:32

    Rais wa Brazil akutwa na Corona

    Rais wa Brazil Jair Bolsonaro ameambukizwa virusi vya corona kwa mujibu wa vipimo vya Madaktari. Rais huyo amesema licha ya kwamba ana dalili za homa na joto kali lakini yupo imara na anaamini virusi hivyo havitomfanya awe hoi na kulazwa Hospitalini na kwamba atapona hivi karibuni.

    Rais huyo aliwahi kunukuliwa akipuuza miongozo ya kujikinga na virusi vya corona ikiwemo kugoma kabisa kuvaa barakoa huku akitoa kauli za kuudharau ugonjwa huo kwa kuuita 'Mafua ya Kawaida'.

    Waziri Mkuu wa Ivory Coast aaga dunia baada ya mkutano wa baraza la mawaziri

    Waziri Mkuu wa Ivory Coast Amadou Coulibaly amefariki baada ya kuugua wakati wa kikao cha baraza la mawaziri.

    Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 61 alikuwa amechaguliwa kuwa mgombea wa chama tawala katika uchaguzi wa mwezi Oktoba, baada ya Alessane Ouattara kusema kuwa hatowania muhula wa tatu.

    Bwana Gon Coulibaly alikuwa amerudi kutoka Ufaransa ambapo alikuwa amepokea matibabu ya moyo kwa miezi miwili.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako