• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 4-Julai 10)

    (GMT+08:00) 2020-07-10 16:09:32

    Virusi vya corona: Kenya yatoa muongozo mpya wa usafiri kudhibiti maambukizi

    Hakutakuwa na haja ya kujitenga kwa lazima kwa wasifiri na watalii wanaowasili nchini Kenya ikiwa hawaoneshi dalili za ugonjwa wa Covid-19, kulingana na tangazo la serikali.

    Kwa mujibu wa Waziri wa Uchukuzi nchini Kenya Bwana James Macharia, abiria wote hawatalazimika kuwekwa kwenye karantini wanapowasili kutoka maeneo waliotoka ikiwa kiwango cha joto la mwili sio zaidi ya nyuzijoto 37.5 na kama hawana kikohozi cha kuendelea, hawana matatizo ya kupumua na wala kuonesha dalili zingine za mafua.

    Ili kuimarisha hatua za usalama za kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19, Waziri wa uchukuzi James Macharia amesema viwanja vya ndege kote nchini vitaruhusiwa tu wafanyakazi na wasafiri pekee isipokuwa kama msafiri anahitaji huduma maalum.

    Bwana Macharia amesema kwamba lengo la hatua zilizochukuliwa ni kuhamasisha watalii ili kuimarisha sekta hiyo ambayo imeporomoka vibaya kipindi hiki cha virusi vya corona.

    Waziri wa uchukuzi pia ametangaza kwamba huduma ya treni ya mwendo kasi 'Madaraka Express' itaanza tena shughuli za uchukuzi Jumatatu kwa safari za miji ya Nairobi na Mombasa mara moja kwa siku.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako