• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 4-Julai 10)

    (GMT+08:00) 2020-07-10 16:09:32

    Tundu Lissu asema atarejea Tanzania Julai 28

    Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amesema anatarajia kurudi nchini humo Julai 28.

    Lissu ametangaza nia ya kugombea urais kupitia chama chake cha CHADEMA Oktoba mwaka huu.

    Mwanasiasa huyo kwa sasa yuko ughaibuni ambapo alienda kupata matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi mwaka 2017.

    Akizungumza mapema wiki hii katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao ulioandaliwa na taasisi ya The Resistance Bureau, Lissu amesema ameshakata tiketi ya ndege na watanzania watarajie kumpokea Julai 28.

    Mjadala huo umewahusisha viongozi kadhaa wa upinzani na wanaharakati mbalimbali wa Afrika, washiriki wa Afrika Mashariki wakiwa Bobi Wine mpinzani kutoka nchini Uganda na Tundu Lissu wa Tanzania

    Akijibu swali kuhusu kama anahofu kuwa anaweza kuzuiwa kuingia nchini mwake, Lisu amesema hana sababu ya kuamini kuwa atazuiwa kurudi nyumbani, akiongeza kuwa yeye si mhalifu. Anasisitiza kuwa aliondoka nje ya Tanzania akiwa hana fahamu, baada ya kushambuliwa kwa risasi mara 16 na watu ambao anasema mpaka sasa hawajakamatwa.

    Juma lililopita Lissu aliwakilishwa na Wakala wake David Djumbe kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama cha CHADEMA kuwania nafasi ya urais.

    Akizungumza kwa njia ya mitandao akiwa ughaibuni, Lissu alitangaza nia ya kuwania urais nchini Tanzania, uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka 2020.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako