• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 10-Oktoba 16)

    (GMT+08:00) 2020-10-16 16:53:39
    Ujerumani yaandikisha idadi kubwa ya maambukizi ya Corona

    Nchi ya Ujerumani imeandikisha idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya virusi vya corona tangu mlipuko huo ulipotokea nchini humo.

    Ndani ya saa 24 zaidi ya watu 6,600 wameripotiwa kupata maambukizi hayo.

    Ripoti hiyo inakuja saa chache tu baada ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kusema kuwa hatua za kukaa nyumbani zitaimarishwa katika baadhi ya maeneo ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

    Hatua hizo ni pamoja na amri ya kutotoka nje wakati wa usiku, ikiwa ni pamoja na marufuku ya pombe na marufuku ya mikusanyiko ya umma.

    Katika nchi jirani ya Ufaransa, kugunduliwa kwa watu 20,000 wenye maambukizi kwa siku moja kulimfanya rais Emmanuel Macron kuweka marufuku ya kutotoka nje usiku mjini paris na miji mingine minane.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako