• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 10-Oktoba 16)

    (GMT+08:00) 2020-10-16 16:53:39
    Nigeria yaendelea kushuudia maandamano

    Maandamano yaliendelea kushuhudiwa nchini Nigeria, kulaani dhulma zinazodaiwa kufanywa na kikosi cha jeshi la Polisi nchini humo kinachojulikana kama SARS. Awali serikali ya Nigeria ilikuwa imeahidi kukifanyia mageuzi na kukivunja kikosi hicho maalum cha SARS kilichokuwa kimepewa kazi ya kupambana na wahalifu. Jumatano, waandamanaji walifunga barabara kuu jijini Lagos, huku wakionekana wenye hasira kwa kile walichokisema kuwa wamechoshwa kuhangaishwa na maafisa wa Polisi. Licha ya serikali Jumapili iliyopita, kutangaza kufutwa kwa kikosi hicho maalum cha polisi kilichopewa kazi ya kupambana na wahalifu katika majimbo mbalimbali, waandamanaji wanasema hawajaridhika na hatua hiyo na hawaiamini serikali na wanachokitaka ni mageuzi katika jeshi hilo.

    Siku ya Jumanne, Mkuu wa Jeshi la Polisi alitangaza kuanziwa kwa kikosi kipya kinachofahamika kama SWAT ambacho sasa kitakuwa na kazi ya kupokonya watu wanaomiliki silaha kinyume na sheria.

    Maandamano pia yameshuhudiwa katika mji mkuu wa Abuja, huku serikali ikisema ina nia ya dhati ya kulifanyia mageuzi jeshi hilo, kauli ambayo imeungwa mkono na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Edward Kallon.

    Tume ya uchumi katika Umoja wa Mataifa imeelezea masikitiko yake kutokana na kushuka kwa mchango wa kifedha unaotumwa nyumbani na raia wa bara Afrika, hii ikihusishwa pakubwa na athari za janga la Corona kwenye chumi nyingi.

    Kwa mujibu wa tume hiyo, wahamiaji kutoka Afrika wamekuwa waathiriwa wa mdororo wa uchumi unaoendelea kushuhudiwa kwenye mataifa mengi kufuatia janga la Corona. Takwimu za Umoja wa Mataifa zimesema kuwa fedha zinazotumwa nyumbani na raia wa Afrika zinatazamiwa kushuka kwa dola bilioni 18 za Marekani, ikilinganishwa na mwaka jana. Tume hiyo imeonya hali hiyo ni tishio kubwa zaidi kwa mataifa yenye mizozo kwani wanaotegemea msaada huo ni wengi mno. Imeomba taasisi za kifedha kupunguza ada za kutuma fedha hizo na mataifa yaliyoendelea kuwajumuisha wahamiaji kwenye mpango wa msaada kwa jamii, ili kunusuru hali.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako