• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 10-Oktoba 16)

    (GMT+08:00) 2020-10-16 16:53:39
    Tanzania kutumia helikopta kuzima moto katika mlima Kilimanjaro

    Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania Dkt Hamisi Kigwangalla amesema upepo mkali na kukauka kwa nyasi na vichaka kumesababisha kusambaa zaidi kwa moto uliotokea Jumapili mchana katika Mlima Kilimanjaro, ambao ni mkubwa kabisa katika Afrika.

    Dkt Kigwangalla ambaye jumatano alifanya ziara ya ukaguzi kwenye eneo lililoungua moto amebainisha kuwa kazi ya kuuzima moto huo ni ngumu na ina changamoto kuliko walivyofikiria. Aidha amesema utaratibu unawekwa wa kutumia helikopta kuzima moto. Amewataka wasamaria wema kuchangia maji na chakula kwa wazima moto 500 na zaidi wanaopambana kuzima moto na pia kuwataka Watanzania kuwaombea wazima moto na watu wengine waliojitolea.

    Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema mbali na moto huo kuharibu msitu na ikolojia ya mlimani, pia umeteketeza vibanda 12, vyoo viwili na vifaa vya umeme wa jua vinavyotumiwa na watalii wanaopanda Mlima Kilimanjaro.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako