![]() Mashairi ya kale ya China ni urithi wenye thamani kubwa sana katika utamaduni wa China, ambayo washairi wa China walieleza matumaini yao kupitia mashairi hayo yenye maneno ya kupendeza yaliyomo, ili kutoa matarajio yao ya kutafuta ukweli, wema na uzuri maishani. Ingawa miaka mingi imeshapita tangu mashairi hayo yalipoanza kuandikwa, lakini bado yanakumbukwa na watu wengi wanaoishi katika zama za hivi leo. Licha ya hayo, kuimba nyimbo zenye mtindo wa kisasa ni njia mpya mwafaka ya kusoma, kufurahia na kueneza mashairi hayo maarufu, ambayo ni njia nzuri ya kuyapatia mashairi hayo ya kale uhai mpya. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo maalumu zilizotungwa kutokana na mashairi ya kale ya China, ili kukufahamisha utamaduni wa mashairi hayo ya China kupitia nyimbo zenye mtindo wa kisasa. |
![]() Katika tarehe 8 mwezi wa nane mwaka 2008, Michezo ya 29 ya Olimpiki ya majira ya joto ilifunguliwa rasmi mjini Beijing, China, ambayo siku hiyo imekuwa kumbukumbu ya kupendeza isiyosahaulika kwa watu wengi. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zilizoanza kusikika miaka kumi kamili iliyopita kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008. |
![]() ![]() Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina yaani sikukuu ya spring ni sikukuu kubwa kabisa kwa Wachina wote katika mwaka mzima. Kila ifikapo sikukuu hiyo muhimu, watu hurudi nyumbani na kujumuika na familia zao ili kusherehekea mwaka mpya, kwa kuwa nyumbani ni mahali penye furaha na upendo. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo mbalimbali zinazohusu sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina. |
![]() ![]() Tarehe 14 ya mwezi Februari ni siku ya wapendanao. Kila ifikapo siku hiyo maalumu, harufu tamu ya mapenzi inatanda kila pembe ya dunia. Ndiyo ni wakati wa kuburudika na kufurahia hisia ya mapenzi matamu maishani. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu mapenzi matamu kati ya wapendanao. |
![]() ![]() Mwaka 2018 umefika, mambo mapya yapo kila pembe ya dunia yetu. Tukumbatie kwa pamoja mwaka mpya wa 2018. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu mwanzo mpya kabisa maishani. |
![]() ![]() Miji mingi hapa China inawavutia watalii wengi duniani kuitembelea. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu miji mbalimabli hapa China. |
![]() ![]() Majira ya baridi hutujia hapa China kila ifikapo mwishoni mwa mwaka mzima. Theluji huanguka katika majira hayo, ambayo inatupatia dunia yenye mandhari nzuri. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu majira ya baridi. |
![]() ![]() Siku ya kuzaliwa ni siku maalumu katika mwaka mzima. Furaha na matumaini mengi hutujia katika siku hiyo, ambayo yanabeba penzi kutoka kwa wale wanaotupenda. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu siku ya kuzaliwa. |
![]() ![]() Kuna watu wengi walioko nje ya nyumbani kwa ajili ya kazi au masomo yao, ambao wanakumbuka nyumbani kwao mara kwa mara. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu kukumbuka nyumbani, na kuwatakia watu hao maisha mema na afya njema nje ya nyumbani. |
![]() ![]() Wakati ni zawadi nzuri kwa kila mtu, ambao unatupatia nafasi nyingi za kutimiza ndoto. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusiana na wakati. |
![]() ![]() Kila Jumapili ya tatu katika mwezi wa sita ni Siku ya Baba. Kila ifikapo siku hiyo maalumu, watoto wanaeleza matumaini yao ya dhati kwa baba zao wapendwa. Mapenzi ya baba ni ya kimyakimya kama mlima mkubwa unaomfuatilia na kumlinda mtoto wake. Na katika kipindi hiki, nyimbo zinazohusu baba zitakuwa zawadi maalumu kwa ajili ya akina baba, ili kuwatakia sikukuu njema na kila la heri. Heri ya Siku ya Baba! "父亲节快乐!fù qīn jié kuài lè !" |
![]() ![]() Kila Jumapili ya pili katika mwezi wa tano ni Siku ya Mama. Kila ifikapo siku hiyo maalumu, watu hupenda kuwasalimia mama zao na kuwapatia zawadi. Na katika kipindi hiki, nyimbo zinazohusu mama zitakuwa zawadi maalumu kwa ajili ya akina mama, ili kuwapatia matumaini yetu mazuri. Heri ya Siku ya Mama! "母亲节快乐!mǔ qīn jié kuài lè !" |
![]() ![]() Kuna nyimbo nyingi zinazotumika kwenye matangazo ya biashara, ambayo yamezifanya nyimbo hizo ziwe umaarufu zaidi kwa wasikilizaji na watazamaji. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo hizo maarufu zilizowahi kutumika kwenye matangazo ya biashara hapa China. |
![]() ![]() Ingawa dunia ni kubwa sana, lakini mioyo yetu inaweza kukutana na kusalimiana, na nyimbo zinazohusu sayari ya dunia hubeba upendo wa maisha. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusiana na sayari ya dunia. |
![]() ![]() Mwimbaji Zhang Guorong (张国荣 zhāng guó róng)ni mwimbaji na mwigizaji maarufu sana hapa China. Ingawa aliaga dunia mwaka 2003, lakini hadi sasa anakumbukwa na mashabiki wake. Nyimbo na filamu zake bado zinapendwa na kusifiwa sana na watu wengi. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo za mwimbaji Zhang Guorong. |
![]() ![]() Watu wengi wanapenda kusikiliza redio, ambayo inaweza kutuunganisha bila ya kujali umbali kati yetu. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu redio. |
![]() ![]() Mashairi yanaweza kutuletea hisia mbalimbali, na watu wengi wanapenda kusoma mashairi. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusiana na mashairi. |
![]() ![]() Tarehe 14 Februari ni siku maalumu, yaani siku ya wapendanao. Mapenzi ni mambo matamu maishani, kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu wapendanao. |
![]() ![]() Kila ifikapo majira ya spring, baridi itaondoka, maua yatachanua tena. Hivyo, majira ya spring pia yanaitwa majira ya mchipuko, ambayo yanamaanisha mambo mapya na mwanzo mpya maishani. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusiana na majira ya spring. |
![]() ![]() Sikukuu ya spring, yaani sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina ni sikukuu kubwa kabisa kwa watu wa China katika mwaka mzima. Katika kalenda ya kichina, mwaka 2017 ni mwaka wa jogoo. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo mbalimbali zinazohusiana na sikukuu ya spring ya China. |
![]() ![]() Marafiki ni watu muhimu katika maisha yetu. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusiana na marafiki. |
![]() ![]() Mwimbaji Li Ronghao(李荣浩 lǐ róng hào)ni mwanamuziki mwenye kipaji kikubwa, nyimbo zake zinavuma sana hivi sasa hapa China. Nyimbo nyingi zinazotungwa naye zina ushawishi mkubwa wa kuwavutia wasikilizaji, maneno yaliyomo kwenye nyimbo zake ni kama mtu anayesimulia hadithi zetu. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo za mwimbaji Li Ronghao. |
![]() ![]() Nyimbo za mapenzi za mwimbaji Xue Zhiqian(薛之谦 xuē zhī qiān)zinaweza kutuonyesha picha mbalimbali zenye rangi na hisia tofauti. Wasikilizaji wengi wanapenda kusikiliza nyimbo zake, kwa sababu nyimbo hizo zinasimulia hadithi zinazotuhusu. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo za mwimbaji Xue Zhiqian. |
![]() ![]() Kuimba nyimbo kunaweza kutuburudisha na kutuletea furaha. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusiana na kuimba. |
![]() ![]() Malaika anabeba upendo kwa maisha yetu. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusiana na malaika. |
![]() ![]() Anga hubeba hisia mbalimbali za binadamu. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusiana na anga. |
![]() ![]() Picha zinatukumbusha mambo au watu fulani, pia ni kumbukumbu ya siku za nyuma. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusiana na picha. |
![]() ![]() Kucheza dansi kunaweza kutuletea fuhara katika maisha yetu, na nyimbo zinazohusu dansi pia zinaweza kutuburudisha. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo mbalimbali zinazohusiana na dansi. |
![]() ![]() Maisha yetu ni kama jukwaa, ambalo linahusiana na ndoto yetu, kila mtu anacheza katika jukwaa lake la kipekee. Tutapata maisha yenye rangi tofauti kwenye jukwaa. Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusu jukwaa la maisha. |
![]() ![]() Ufunguo ni kitu cha kawaida katika maisha yetu, na waimbaji wanapenda kutumia ufunguo ili kutoa hisia ya maisha, hasa kwa mambo ya mapenzi.Kipindi hiki kitakuletea nyimbo zinazohusiana na ufunguo. |
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |