Tona anatoka Zimbabwe. Amesoma katika Chuo Kikuu cha Zhejiang kwa miaka miwili, na hivi sasa anasomea shahada ya udaktari wa kozi ya usalama usio wa kijadi wa usimamizi wa umma. Alisema, baba yake aliwahi kutembelea nchini China, hivyo aliona picha za China kutoka kwake. Lakini hakutarajia kuwa China imekuwa na mabadiliko makubwa namna hii. Anapenda sana mji wa Hangzhou, kwani katika mji huo hakuna makelele, lakini hauwafanyi watu waone upweke, mbali na hayo, mji huo una mandhari nzuri na watu wapole wenye moyo mwema.
Louis anatoka Liberia. Ameishi mjini Hangzhou kwa miaka miwili, na hivi sasa anasomea kozi ya usimamizi wa nguvu kazi kwenye Chuo Kikuu cha Zhejiang. Anasema, "Ninajihisi maisha mapya nchini China. Mji wa Hangzhou ni mji mzuri, katika mji huo, watu wanaweza kuona Ziwa Xihu na kujihisi kitu muhimu zaidi cha maisha. Ninyi nyote marafiki zangu, mje hapa kutimiza ndoto yenu ya kuishi maisha bora. Ndugu zetu wakarimu wa China watawapa msaada wa kirafiki wakati wowote mnapohitaji.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |