Muda mfupi baada ya kuja hapa China, nilikwenda jumba la michezo lililoko karibu na chuo chetu kutazama mashindano ya soka pamoja na rafiki yangu mmoja kutoka Senegal. Sikujua kuwa timu hizo mbili zilitoka wapi, lakini zilicheza vizuri, na mashabiki wao waliishangilia timu zao kwa njia mbalimbali. Pia tulikutana na marafiki kadhaa wa China, tulitazama mashindano na kuzungumza pamoja, na tulikuwa na wakati mzuri kwa pamoja. Kusema kweli, napenda zaidi kucheza mchezo wa Rugby, hii ndiyo sababu kuwa nina afya nzuri. Lakini niliumia mguu kabla ya kuja hapa Hangzhou, hivyo siwezi kucheza mpira huo sasa. Ninaamini kuwa iko siku nitarudi kiwanjani kucheza mpira huo baada ya kupona. Licha ya mipira, pia ninapenda kuimba nyimbo na kupiga ala za muziki. Lakini jambo ninalopenda zaidi ni kusoma kozi yangu ya usalama usio wa jadi, kwani ninataka kufanya dunia yetu iwe nzuri na yenye usalama zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |