4: Maingiliano na Nchi za Nje

Ujulisho Mfupi Kuhusu Hali ya Kidiplomasia

Jamhuri ya Watu wa China iliyozaliwa mwaka 1949, ilifungua ukurasa mpya wa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na nchi mbalimbali duniani.

Kuanzia mwaka 1949 hadi mwishoni mwa miaka ya 50 ya karne iliyopita, China na Urusi ya zamani na nchi mbalimbali za kijamaa zilianzisha uhusiano wa kibalozi na kuendeleza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano. Baada ya kufanyika kwa Mkutano wa Asia na Afrika wa Bandung, Indonesia mwaka 1955, nchi kadhaa za Asia na Afrika zilianzisha uhusiano wa kibalozi na China. Ilipofika mwaka 1956, nchi 25 duniani ziliwekeana uhusiano wa kibalozi na China.

Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 50 hadi mwishoni mwa miaka ya 60 ya karne iliyopita kwa nyakati tofauti, China na nchi za Guinea, Ghana, Mali, Congo na Tanzania zilisaini mikataba ya urafiki na mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia, ambapo China iliunga mkono mapambano ya kujipatia uhuru yaliyofanywa na Angola, Guinea Bissau, Msumbiji, Zimbabwe na Namibia na kuunga mkono mapambano yaliyofanywa na wananchi wa Afrika ya kusini kupinga ubaguzi wa rangi wa walowezi. China ilitatua masuala ya mipaka yaliyobaki katika historia kati yake na Myanmar, Nepal, Mongolia na Afghanistan, na kusaini mikataba ya mipaka; China na Pakistan zilisaini mkataba wa mipaka kati ya sehemu ya Xinjiang ya China na sehemu ambayo ulinzi wake halisi unadhibitiwa na Pakistan; China na Indonesia zilitatua suala kuhusu wachina wenye uraia wa nchi mbili walioishi nchini Indonesia. Ilipofika mwaka 1969, nchi zilizowekeana na China uhusiano wa kibalozi zilifikia 50.

Mwezi Oktoba mwaka 1971, chini ya uungaji mkono wa nchi nyingi zinazoendelea, Baraza kuu la 26 la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la No.2758 kwa kura nyingi kabisa za ndio kurudisha haki zote halali za Jamhuri ya Watu wa China katika Umoja wa Mataifa, na kumwondoa mara moja mwakilishi wa kundi la Chama cha Guomintang kutoka Umoja wa Mataifa na mashirika yote ya umoja huo. Tangu hapo China ikaanzisha uhusiano wa kibalozi na nchi nyingi kabisa za magharibi, na kufungua ukurasa mpya wa mambo ya kidiplomasia.

Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 70 hadi miaka ya 80 ya karne iliyopita, chini ya uelekezaji wa fikra ya Deng Xiaoping kuhusu mambo ya kidiplomasia, China iliendeleza uhusiano na nchi za dunia ya tatu. Kuboresha na kuendeleza uhusiano na nchi jirani na nchi nyingi zinazoendelea. Ili kutatua ipasavyo suala la Hongkong na suala la Makau, China ilifanya mazungumzo ya kidiplomaisa na Uingereza na Ureno, kwa nyakati tofauti China na nchi hizo mbili zilitoa taarifa ya pamoja mwezi Disemba mwaka 1984 na mwezi Aprili mwaka 1987, ambapo zilithibitisha mambo kuhusu serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kurudisha mamlaka yake huko Hong kong na Makau tarehe 1 Julai mwaka 1997 na tarehe 20 Desemba mwaka 1999.

Kuanzia miaka ya 90 ya karne iliyopita, viongozi wa awamu ya tatu wa China wakiongozwa na Jiang Zemin walirithi na kutekeleza fikra ya Deng Xiaoping kuhusu mambo ya diplomasia na sera ya kidiplomasia ya amani ya China iliyo ya kujitawala na kujiamulia, kufanya juhudi kuendeleza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano na nchi mbalimbali duniani kwenye msingi wa kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani, na kusukuma mbele kwa pamoja kuanzishwa kwa utaratibu mpya wa kisiasa na kiuchumi duniani. Wakati huo China ilifufua uhusiano wa kibalozi na Indonesia, kuanzisha uhusiano wa kibalozi na Singapore, Brunei na Korea ya kusini, na kuufanya uhusiano kati yake na Vietnam na Mongolia kuwa wa kawaida.

Mwaka 1996, rais wa wakati huo wa China Jiang Zemin alifanya ziara katika nchi 3 za Asia ya kusini, baada ya kufanya mashauriano, China na nchi hizo ziliamua kuwa China na India kuanzisha uhusiano wa kiwenzi wa kuelekea karne ya 21, China na Pakistan kuanzisha uhusiano wa kiwenzi wa ushirikiano kwenye sekta zote wa kuelekea karne ya 21, na China na Nepal kuanzisha uhusiano wa urafiki na ujirani mwema wa vizazi hadi vizazi. China ilifanya juhudi kuendeleza uhusiano na nchi za Asia, Afrika na Latin Amerika na Ulaya ya mashariki na kati. Uhusiano kati ya China na nchi za kusini mwa Sahara na kusini mwa Afrika umeimarishwa zaidi. Uhusiano kati ya China na Latin Amerika unaendelea siku hadi siku. Nchi za Latin Amerika zilizowekeana uhusiano wa kibalozi na China ziliongezeka na kufikia 19. Nchi kadhaa ambazo zilikuwa bado hazijawekeana uhusiano wa kibalozi na China pia zilianza kuzingatia kuendeleza uhusiano kati yao na China.

Binadamu waliingia karne mpya ya 21, ambapo kuna ncha nyingi duniani, na utandawazi wa uchumi unaendelea siku hadi siku duniani. China ni nchi inayoendelea, idadi ya watu wake ni kubwa zaidi kuliko nchi nyingine duniani. Maendeleo ya China hayawezi kutengana na dunia, na maendeleo ya dunia yanahitaji China. China inatumai kidhati kuimarisha ushirikiano na nchi na sehemu zote kwenye msingi wa kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani, ili kupata maendeleo kwa pamoja.


1 2 3 4 5 6 7