4: Maingiliano na Nchi za Nje

Uhusiano kati ya China na Marekani, Japan na Russia]

Uhusiano Kati ya China na Marekani

Mwezi Februari, 1972, rais Richard Nixon wa Marekani alifanya ziara nchini China, ambapo ilitolewa Taarifa ya pamoja ya China na Marekani (yaani "Taarifa ya Shanghai"), ambayo ilionesha kumalizika kwa hali ya kutengana kabisa kati ya China na Marekani kwa zaidi ya miaka 20. Tarehe 16 Desemba, 1978, ilitolewa "Taarifa ya pamoja ya Jamhuri ya watu wa China na Marekani kuwekeana uhusiano wa kibalozi". Tarehe 1 Januari, 1979, China na Marekani zilianzisha rasmi uhusiano wa kibalozi. Tarehe 17 Agosti 1982, China na Marekani zilitoa "Taarifa ya 8.17" ambayo imeweka kanuni kuhusu Marekani kuiuzia Taiwan silaha, yaani kutatua hatua kwa hatua suala hilo mpaka litatuliwe kabisa.

Mwezi Januari 1984, waziri mkuu wa China Li Peng alifanya ziara nchini Marekani, mwezi Aprili mwaka huo, rais Ronald Reagan alifanya ziara nchini China. Mwezi Julai, 1985, rais Li Xiannia wa China alifanya ziara nchini Marekani. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa rais wa China kuitembelea Marekani.

Mwezi Januari 1998 waziri wa ulinzi wa taifa wa Marekani William Kohen alifanya ziara nchini China, ambapo China na Marekani zilisaini "Mkataba wa wizara za ulinzi wa taifa za China na Marekani kuhusu kuanzisha utaratibu wa kuimarisha mashauriano ya usalama wa kijeshi kwenye bahari". Tarehe 25,Mei mwaka huo, rais Jiang Zemin na rais Bill Clinton kwa mara ya kwanza walianzisha mawasiliano ya kuongea kwa simu moja kwa moja, siku hiyo walizungumzia hali ya Asia ya kusini na uhusiano kati ya China na Marekani.

Tarehe 25 Juni hadi tarehe 3 Julai mwaka 1998, kutokana na mwaliko wa rais Jiang Zemin, Rais Bill Clinton alifanya ziara nchini China, ambapo marais hao wawili walikuwa na mazungumzo na walikubaliana kuwa China na Marekani zitaimarisha zaidi mazungumzo na ushirikiano kuhusu masuala makubwa ya kimataifa; China na Marekani zimekubaliana kuendelea na juhudi za pamoja na kupiga hatua kubwa kwa lengo la kujenga uhusaino wa kiwenzi na kimkakati unaoelekea karne ya 21. Pande hizo mbili zimeamua kuwa, silaha za nyuklia za kimkakati zinazodhibitiwa na kila upande hazitaulenga upande mwingine; na kukubali kuimarisha zaidi mazungumzo ya kimkakati kwenye sekta za uchumi na fedha ili kutoa mchango mkubwa katika kusukuma mbele maendeleo mazuri ya uchumi wa dunia na fedha za kimataifa.

Tarehe 1 Januari, 1999, rais Jiang Zemin na rais Clinton walitumiana salamu za kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani. Tarehe 6 hadi 14 Aprili mwaka huo, waziri mkuu wa China Zhu Ronji alifanya ziara rasmi nchini Marekani. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa waziri mkuu wa China kuitembelea Marekani miaka 15 iliyopita.

Tarehe 8 Mei, 1999, saa 11 na dakika 45 ya saa za Beijing, Jumuia ya NATO inayoongozwa na Marekani ilirusha makombora matano kutoka pande tofauti dhidi ya ubalozi wa China nchini Jamhuri ya shirikisho la Yugoslavia, ambapo waandishi watatu wa habari wa China waliuawa, wafanyakazi wengine wa ubalozi huo zaidi ya 20 walijeruhiwa, na jengo la ubalozi huo liliharibiwa vibaya. Wananchi wa China walikuwa na ghadhabu kubwa sana juu ya vitendo hivyo viovu vya Marekani, ambapo uhusiano kati ya China na Marekani uliathiriwa kwa kiasi fulani.

Tarehe 11 Septemba mwaka huo, rais Jiang Zemin na rais Clinton walikuwa na mazungumzo wakati mkutano usio rasmi wa viongozi wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki ulipofanyika huko Aukland, New Zealand, mazungumzo hayo yalipata matokeo yenye juhudi.

Mwaka 2000, mawasiliano kati ya viongozi na ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya China na Marekani uliongezeka. Tarehe 15 Desemba mwaka huo, bunge la Marekani lilipitisha "sheria ya utengaji wa fedha" likafanya mpango wa kufidia dola za kimarekani milioni 2800 kwa hasara za mali za ubalozi wa China nchini Yugoslavia kutokana na mashambalizi ya makombora ya Marekani.

Tarehe 1 Aprili, 2001, ndege moja ya upelelezi wa kijeshi ya aina ya EP-3 ya Marekani ilipofanya upelelezi kwenye anga ya China katika sehemu ya bahari ya umbali wa kilomita 104 toka kusini mashariki ya Kisiwa cha Hainan,China, iligongana na ndege moja ya China iliyoifuata na kuiagusha, ikamfanya rubani wa ndege hiyo ya China Wang Wei kufa papo hapo. Baada ya kuzusha ajali hiyo, ndege hiyo ya Marekani iliingia anga ya mamlaka ya China bila kupata ruhusa, na kutua kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi wa Linshui, kisiwani Hainan, China. Tarehe 11 Aprili, waziri wa mambo ya nje wa China Bwana Tang Jiashuan alipokea barua ya kuomba radhi kutoka kwa mwakilishi wa serikali ya Marekani ambaye alikuwa balozi wa Marekani nchini China.

Tarehe 11 Septemba mwaka huo, sehemu za New York na Washington za Marekani zilishambuliwa na ugaidi wa kimabavu, na kusababisha vifo na majeruhi wa watu wengi na hasara kubwa za mali. Tarehe 19 Oktoba, rais Jiang Zemin na rais Bush walikutana huko Shanghai, wakibadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani, mapambano dhidi ya ugaidi na masuala mengine makubwa, na walifikia maoni muhimu ya pamoja. Pande hizo mbili zilikubali kwa kauli moja kufanya juhudi za pamoja kwa kuendeleza uhusiano wa ushirikiano wa kiujenzi kati ya China na Marekani.

Mwaka 2002, maendelo ya uhusiano kati ya China na Marekani yalikumbwa na usumbufu kadha wa kadha, lakini kwa ujumla uhusiano huo ulidumisha mwelekeo wa kuboreshwa na kukuzwa. Tarehe 21 hadi 22 Februari, kutokana na mwaliko wa rais Jiang Zemin, rais Bush alifanya ziara nchini China. Marais wa nchi hizo mbili walikutana tena na kujadili kwa kina uhusiano wa pande mbili na hali ya kimataifa, na walikubali kwa kauli moja kuimarisha mazungumzo na ushirikiano kati ya China na Marekani, kushughulikia mwafaka migongano na kufanya juhudi kwa pamoja kusukuma mbele maendeleo ya ushirikiano wa kiujenzi kati ya China na Marekani. Rais Jiang Zemin alipokea mwaliko wa rais Bush, akafanya ziara nchini Marekani mwezi Oktoba kabla ya kwenda Mexico kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa Asia na Pasifiki. Rais Jiang Zeming alisisitiza kwa rais Bush kuwa kutatua mwafaka suala la Taiwan kuna umuhimu mkubwa kwa kuendeleza uhusiano kati ya China na Marekani. Rais Bush alisisitiza kuwa Marekani inafuata sera ya kuwepo kwa China moja na kufuata taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, hii ni sera inayofuatwa siku zote na serikali ya Marekani, ambayo haibadiliki.

Uhusiano Kati ya China na Japan    

Tarehe 2 Oktoba, 1971, kisiasa, China ilitoa "kanuni tatu za kurudisha uhusiano wa kibalozi kati ya China na Japan", yaani Jamhuri ya watu wa China ni serikali pekee halali inayoiwakilisha China; Taiwan ni sehemu moja isiyotengeka ya ardhi ya Jamhuri ya watu wa China; "Mkataba wa amani wa Japan na Chang Keishek" ni haramu ambao hauwezi kufanya kazi, lazima ufutwe. Tarehe 25 Septemba, 1972, waziri mkuu wa Japan Tanaka Kakoei alifanya ziara nchini China, tarehe 29 serikali za China na Japan zilitoa taarifa ya pamoja, na China na Japan ziliufanya uhusiano wa kibalozi uwe wa kawaida.

Hivi sasa uhusiano kati ya China na Japan unadumisha maendeleo kwa ujumla, ambapo matokeo yenye juhudi yamepatikana katika ushirikiano halisi kwenye sekta mbalimbali. Lakini kwa upande mwingine, waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi alikwenda mara kwa mara hekalu kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita, hili limekuwa tatizo kubwa la kuathiri vibaya uhusiano wa kisiasa kati ya China na Japan.

Kiuchumi, China na Japan zimekuwa wenzi wakubwa wa kibiashara. Japan imekuwa mwenzi mkubwa kabisa wa China katika shughuli za biashara kwa miaka mfululizo, na China imekuwa nchi ya pili inayofanya biashara kwa wingi na Japan, ambapo China imekuwa soko kubwa la pili kwa Japan kusafirisha bidhaa nje.

Katika ushirikiano katika sekta za sayansi, elimu, utamaduni na afya, baada ya uhusiano kati ya China na Japan kuwa wa kawaida, pande hizo mbili zimeanzisha ushirikiano wa kiserikali katika mambo ya sayansi na teknolojia, na kusaini "mkataba wa ushirikiano wa kisayansi na kiteknolojia wa China na Japan" mwezi Mei, 1980. Tangu hapo, mawasiliano na ushirikiano wa kisayansi na kiteknolojia kati ya nchi hizo mbili yameendelea kwa haraka na kupanuliwa siku hadi siku kwenye ngazi mbalimbali na kwa aina nyingi.

Tarehe 6 Desemba, 1979, China na Japan zilisaini "Mkataba wa maingiliano ya kiutamaduni kati ya China na Japan", kukubali kuendeleza mawasiliano kati ya nchi hizo mbili kwenye sekta za utamaduni, elimu, taalum na michezo. Mwaka 2002 serikali za nchi hizo mbili ziliamua kuanzisha shughuli mbalimbali za maingiliano kama vile "Mwaka wa utamaduni wa China" na "Mwaka wa utamaduni wa Japan", "Mashindano ya chemsha bongo ya ujuzi kwenye televisheni" na "Baraza la uchumi la China na Japan".

Hivi sasa kuhusu uhusiano kati ya China na Japan, bado kuna masuala mengi nyeti yanayostahili kushughulikiwa kwa makini:

Kwanza ni suala la kutambua historia. Hili ni suala nyeti la kisiasa katika uhusiano kati ya China na Japan. Tokea mwaka 2001, matukio ya kuchapisha vitabu vya mafunzo ya historia iliyorekebishwa na kupotoshwa na Japan bila kujali ukweli wa mambo ya historia, matukio ya kupotosha historia ya uvamizi wa Japan dhidi ya China, na matukio ya waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi kwenda hekalu kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita yalitokea mara kwa mara, ambayo yamezuia vibaya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Japan.

Pili ni suala la Taiwan. China inashikilia msimamo wazi kuhusu uhusiano kati ya Japan na Taiwan, yaani haipingi mawasialino ya kiraia kati ya Japan na Taiwan, lakini inapinga kithabiti Japan kufanya mawasiliano ya kiserikali ya aina yoyote na Taiwan, kufanya "China mbili" au "China moja, Taiwan moja", ikiitaka Japan iahidi bayana Taiwan haipo kwenye ushirikiano kati ya Japan na Marekani katika sekta ya usalama.

Tatu ni suala la Visiwa vya Diaoyu. Visiwa vya Diaoyu viko kwenye eneo la bahari ya mashariki yenye maili 92 toka kaskazini mashariki ya mji wa Jilong wa mkoa wa Taiwan wa China, ambavyo viliundwa na visiwa vya Diaoyu, Huangwei, Chiwei, Naixiao na Beixiao pamoja na miamba kadhaa, visiwa hivyo viko karibu sana na Kisiwa cha Taiwan, navyo ni ardhi ya China tangu enzi na dahari, ni sehemu moja isiyotengeka ya ardhi ya China kama Taiwan ilivyo. China inamiliki mamlaka isiyonyimika kwenye visiwa hivyo na eneo la bahari lililo karibu navyo.

Msimamo huo wa China unategemea ushahidi wa kutosha wa kihistoria na kisheria. Mwezi Desemba, 1943, "Taarifa ya Cairo" iliyotolewa na China, Marekani na Uingereza ilieleza kuwa, Japan inapaswa kuirudishia China ardhi ilizoiba kutoka China zikiwa pamoja na sehemu ya kaskazini mashariki ya China, Kisiwa cha Taiwan, na Visiwa vya Penghu. "Tangazo la Potsdam" la mwaka 1945 lilieza kuwa, "sharti lililowekwa kwenye Taarifa ya Cairo lazima litekelezwe". Mwezi Agosti mwaka huo, Japan ilipokea "Tangazo la Potsdam" na kutangaza kusalimu amri bila masharti, hii imemaanisha kuwa Japan itairudishia China Kisiwa cha Taiwan na Visiwa vya Diaoyu vilivyo karibu nacho.

Nne ni suala la ushirikiano kati ya Japan na Marekani katika sekta ya usalama. Mwaka 1996 Japan na Marekani zilitoa "Taarifa ya pamoja ya ushirikiano wa kiusalama", kutokana na taarifa hiyo, pande hizo mbili zilianza kurekebisha "Mwongozo wa ushirikiano wa ulinzi" uliotungwa mwaka 1978. Mwezi Septemba, 1997, Japan na Marekani zilithibitisha rasmi mwongozo mpya wa ushirikiano wa kiusalama. Tarehe 24, Mei mwaka 2004, Bunge la Japan lilithibitisha mswada wa sheria unaohusika na mwongozo mpya wa ushirikiano wa kiusalama wa Japan na Marekani, hii imeonesha kuwa utaratibu mpya wa Japan na Marekani katika kuimarisha ushirikiano wa kiusalama umewekwa kimsingi. Juu ya hiyo, China inafuatilia zaidi mwelekeo wake unaohusika na suala la Taiwan, na mwelekeo wake wa kijeshi wa Japan. Mpaka sasa kwa njia mbalimbali China imeeleza ufuatiliaji wake mkubwa na msimamo husika.

Tano ni suala la utoaji fidia wa kivita. Serikali ya Japan ilipofanya mazungumzo na China kuhusu kuufanya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Japan uwe wa kawaida ilieleza wazi kuwa, imeona inawajibika sana na madhara makubwa kwa wananchi wa China kutokana na vita vyake vya uvamizi, na ilijikosoa kwa makini. Kwa msingi huo, serikali ya China ikizingatia maslahi ya kimsingi ya taifa iliamua kuacha ombi la kufidiwa kutokana na hasasa ilizopata kwenye vita, uamuzi huo uliwekwa kwenye "Taarifa ya pamoja ya China na Japan" iliyosainiwa mwaka 1972. Mwaka 1978, "Mkataba wa amani na urafiki wa China na Japan" ulioidhinishwa kwenye mkutano wa 3 wa bunge la 5 la umma la China ulithibitisha tena kwenye waraka wake wa sheria kuhusu uamuzi wa China wa kuacha kudai fidia kutokana na hasara ilizopata kwenye vita vilivyoanzishwa na Japan.

Sita ni suala kuhusu silaha za kikemikali za Japan zilizoachwa kwenye sehemu ya kaskazini ya China. Wakati wa vita vya kuivamia China, Japan ilifika hadi kukiuka mkataba wa kimataifa, ilitumia silaha za kikemikali na kusababisha vifo na majeruhi wa askari na raia wengi wa China. Jeshi la Japan liliposhindwa katika vita, lilizika na kuacha silaha nyingi za kikemikali katika sehemu lililokalia. Mpaka sasa katika zaidi ya sehemu 30 za mikoa na miji ya China ziligunduliwa silaha hizo zilizoachwa na jeshi la Japan. Katika miaka mingi iliyopita, silaha hizo zimeharibiwa vibaya na kutu, hata zilivuja kila mara, zikaleta tishio kubwa dhidi ya usalama wa maisha na mali za wananchi wa China na mazingira ya viumbe. Serikali ya China ilitoa mashitaka rasmi kwa serikali ya Japan mwishoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, na kuitaka serikali ya Japan itatue suala hilo. Tarehe 30 Julai mwaka 1999, serikali za nchi mbili China na Japan zilisaini "Barua ya kumbukumbu kuhusu kuteketeza silaha za kikemikali zilizoachwa na Japan nchini China". Katika barua hiyo, serikali ya Japan iliahidi kukumbuka vizuri "Taarifa ya pamoja ya China na Japan" na "Mkataba wa amani na urafiki wa China na Japan", ikisema imetambua haja ya dharura ya kutatua suala hilo, na kuahidi kutekeleza jukumu lake la kuteketeza silaha hizo kutokana na "Mkataba wa kupiga marufuku silaha za kikemikali". Hivi sasa idara husika za serikali za China na Japan zikifuata barua ya kumbukumbu zinafanya majadiliano kuhusu namna zitakavyoteketezwa haraka iwezekanavyo silaha zilizoachwa na Japan nchini China.

Uhusiano Kati ya China na Russia    

Tarehe 2 Oktoba, 1949, China na Urusi ziliwekeana uhusiano wa kibalozi. Mwezi Agosti, 1991, Shirikisho la Urusi lilisamblatika, tarehe 27 Desemba mwaka huo, China na Russia zilisaini kumbukumbu ya mazungumzo na kuondoa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Urusi ya zamani. Mwaka 2001, uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Russia ulifikia kiwango kipya, ambapo uaminifu wa kisiasa kati ya pande hizo mbili uliongezeka, na mawasiliano kati ya viongozi wakuu yamezidi kuwa barabara zaidi. Rais Jiang Zemin na rais Vladimir Putin walikutana mara tatu mwaka huo, na kuongea kwa simu mara 6. Mkataba wa ujirani mwema, urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili uliosainiwa mwaka 2001 pamoja na taarifa ya pamoja iliyotolewa mwaka huo zilithibitisha kwa njia ya kisheria wazo la amani la kuweka urafiki vizazi hadi vizazi, na daima kutofanya uhasama kati ya nchi hizo mbili na wananchi wa nchi hizo mbili.

Tarehe 26 hadi 28 Mei, 2003, rais Hu Jintao wa China alifanya ziara nchini Russia.

Katika maika ya hivi karibuni, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia kati ya nchi hizo mbili umeimarishwa siku hadi siku. Nchi hizo mbili zimeongeza zaidi siku hadi siku mawasiliano na ushirikiano katika sekta za utamaduni, sayansi na teknolojia na elimu. Na vikundi vya nyimbo na ngoma vya China na Russia vimetembeleana na kufanya maonesho mara kwa mara.

Kuhusu suala la mipaka. Mpaka kati ya China na Russia una urefu wa kilomita 4370 . Kuna tatizo la mipaka lililobaki katika historia kati ya nchi hizo mbili. Nchi hizo mbili zikifuata mkataba wa hivi sasa kuhusu mipaka ya nchi hizo mbili, na kufuata kanuni za sheria ya kimataifa zilizotambuliwa duniani, zimefanya mazungumzo ya miaka mingi, kushauriana kwa usawa, kuelewana na kulegeza masharti, zikathibitisha mwelekeo wa 97 % ya mstari wa mipaka.

Hivi sasa bado haujathibitisha mwelekeo wa mstari wa mpaka wa sehemu mbili za Kisiwa cha Heixiazi na Abageituzhouzhu zilizoko mashariki ya mpaka kati ya China na Russia, pande hizo mbili zitafuata kanuni ya haki na usawa, kuelewana na kurudi nyuma, kutatua haraka iwezekanavyo tatizo la mipaka lililobaki.


1 2 3 4 5 6 7