4: Maingiliano na Nchi za Nje

China na Jumuiya za kimataifa

Umoja wa Asia Kusini Mashariki na China      

Umoja wa nchi za Asia kusini mashariki ulikuwa Umoja wa Asia ya kusini mashariki ulioanzishwa tarehe 31 Julai, 1961. Mwezi Agosit, 1967, nchi tano za Indonesia, Thailand, Singapore, Philippines na Malaysia zilifanya mkutano huko Bangkok na kutoa Taarifa ya Bangkok, zikatangaza kuanzishwa kwa umoja huo. Baadaye nchi tatu za Malaysia, Thailand na Philippines zilifanya mkutano wa mawaziri huko Kuala Lumpur na kuamua kuanzisha Umoja wa nchi za Asia ya kusini mashariki badala ya Umoja wa Asia ya kusini mashariki.

Nia ya umoja huo:

Kufuata moyo wa usawa na ushirikiano, kufanya juhudi za pamoja kwa kuhimiza ongezeko la uchumi, maendeleo ya jamii na utamaduni ya sehemu hiyo.

Kufuata haki, kanuni za uhusiano kati ya nchi na nchi na "Katiba ya Umoja wa Mataifa", kuhimiza amani na utulivu wa sehemu hiyo.

Kuhimiza ushirikiano na kusaidiana katika sekta za uchumi, jamii, utamaduni, teknolojia na sayansi.

Kusaidiana katika mambo ya elimu, mafunzo ya kazi na ufundi pamoja na mambo ya utawala na majengo ya utafiti yanayohusika.

Kufanya ushirikaino wenye ufanisi zaidi katika kutumia ipasavyo kilimo na viwanda, kupanua biashara, kuboresha mawasiliano na uchukuzi, na kuinua kiwango cha maisha ya wananchi.

Kuhimiza utafiti kuhusu masuala ya Asia ya kusini mashariki.

Kudumisha ushirikiano barabara wa kunufaishana na jumuia za kimataifa na kikanda zenye nia na malengo yanayofanana, na kutafuta njia ya kuzidisha zaidi ushirikiano nazo.

Wanachama:

Umoja wa nchi za Asia kusini mashariki una nchi wanachama 10 za Brunei, Cambodia, Indonesia, Laos, Malaysia, Myanmar, Philippines, Singapore, Thailand na Vietnam.

Uhusiano na China:

China imeanzisha uhusiano wa kibalozi na nchi zote wanachama wa Umoja wa Asia kusini mashariki, na mwaka 1996 China imekuwa nchi mwenzi wa umoja huo wa kufanya mazungumzo kwa pande zote.

Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na China     

Mwezi Julai, 2001, marais wa nchi 6 za China, Russia, Kazakstan, Kyrgyzstan, Tajikstan na Uzbekstan walikutana huko Shanghai,China na kusaini "Taarifa ya kuanzishwa kwa Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai", wakitangaza kuanzisha jumuia mpya ya kikanda ya ushirikiano wa pande nyingi. Nia ya jumuia hiyo ni kuimarisha uaminifu na ujirani mwema na urafiki kati ya nchi wanachama; kuzitia moyo nchi wanachama zifanye ushirikiano wenye ufanisi katika sekta za siasa, uchumi na biashara, sayansi na teknolojia, utamaduni, elimu, nishati, mawasiliano na hifadhi ya mazingira; kufanya juhudi za pamoja katika kulinda amani, usalama na utulivu wa dunia na kanda hiyo; kuanzisha utaratibu mpya wa kisiasa na kiuchumi ulio wa kidemokrasia, haki na halali duniani. Pande mbalimbali ziliamua kuanzisha sekretariati ya jumuiya hiyo mjini Beijing.

China ikiwa moja ya nchi zilizopendekeza na kufanya juhudi za kuanzisha Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai, imeshiriki shughuli mbalimbali kwenye jumuia hiyo, kutoa mapendekezo na kanuni nyingi za kiujenzi kwa kuendeleza jumuia hiyo na kutoa mchango mkubwa.

Umoja wa Mataifa na China

Tarehe 25,Aprili, 1945, wajumbe kutoka nchi 50 walifanya mkutano wa jumuia za kimataifa wa Umoja wa Mataifa. Tarehe 25 Juni, ilipitishwa "Katiba ya Umoja wa Mataifa". Tarehe 26 Juni, baada ya China, Ufaransa, Urusi, Uingereza, Marekani na nchi nyingi zilizosaini katiba hiyo kukabidhi barua za kuidhinisha katiba hiyo, katiba hiyo ilianza kufanya kazi, na Umoja wa Matafia ulianzishwa rasmi. Mwaka 1947, Baraza kuu la Umoja wa Mataifa liliamua kuwa, tarehe 24 Oktoba iwe siku ya Umoja wa Mataifa.

Nia ya Umoja wa Mataifa ni: Kulinda amani na usalama wa kimataifa; kuendeleza uhusiano wa kirafiki kwenye msingi wa kuheshimu haki za usawa na kanuni za kujiamulia za wananchi wa nchi mbalimbali; kufanya ushirikiano wa kimataifa, ili kutatua masuala ya kimataifa kuhusu uchumi, jamii, utamaduni na ya kibinadamu, na kuhimiza kuheshimu haki za binadamu na uhuru wa kimsingi wa binadamu wote. Ilipofika mwezi Septemba mwaka 2002, Umoja wa Mataifa ulikuwa na nchi wanachama 191, zikiwemo nchi wanachama waanzilishi 49. Makao makuu ya Umoja wa Mataifa yako New York, Marekani, na ofisi zake nyingine ziko Geneva nchini Uswisi, Vienna nchini Austria, Nairobi nchini Kenya na Bangkok nchini Thailand.

China ni nchi kubwa inayoendelea, pia ni nchi mjumbe wa kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. China siku zote inashikilia kanuni na kutetea haki katika mambo ya kimataifa, na imekuwa na hadhi muhimu maalum katika Umoja wa Mataifa na jukwaa la kimataifa. Hivi sasa Umoja wa Mataifa unaonesha umuhimu gani katika kusukuma mbele kazi ya kujenga utaratibu mpya wa kisiasa na kiuchumi ulio wa haki na halali duniani, hili ni jambo linalofuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Pendekezo la China kuhusu kujenga utaratibu huo, kulinda amani na kusukuma mbele maendeleo na kupinga umwamba linasisitiza usawazishaji na ushirikiano kati ya nchi 5 wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama ili kusaidia amani na maendeleo ya dunia.

Jumuiya ya APEC na China    

Mwezi Januari, 1989, waziri mkuu wa Australia Houk alipoitembelea Korea ya kusini alitoa "pendekezo la Seoul" likishauri kuitisha mkutano wa mawaziri wa sehemu ya Asia na Pasifiki, ili kujadili kuimarisha suala la ushirikiano wa kiuchumi. Baada ya kufanya majadiliano na nchi husika, Australia, Marekani, Japan, Korea ya kusini, New Zealand, Canada na nchi 6 za Umoja wa Asia ya kusini mashariki zilifanya mkutano wa kwanza wa mawaziri wa Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi Asia na Pasifiki huko Canberra, mji mkuu wa Australia, tangu hapo Jumuiya ya APEC ikaanzishwa rasmi.

Mkutano wa 3 wa mawaziri wa APEC ulifanyika mwezi Novemba, 1991 na kupitisha "Taarifa ya Seoul", taarifa hiyo ilithibitisha rasmi nia na lengo la APEC kuwa ni : Kudumisha ongezeko na maendeleo ya uchumi kwa ajili ya maslahi ya pamoja ya wananchi wa sehemu hiyo; kuhimiza uchumi unaosaidiana na kutegemeana kati ya nchi wanachama; kuimarisha utaratibu wa biashara ya pande nyingi na ya ufunguaji mlango; na kupunguza vikwazo vya biashara na uwekezaji wa kikanda.

Jumuiya ya APEC ina nchi 21 wanachama.

Uhusiano kati ya APEC na China

Tangu ijiunge na APEC mwaka 1991, China imefanya juhudi kushiriki katika shughuli mbalimbali za APEC na kuweka mazingira mazuri ya nje kwa mageuzi na ufunguaji mlango wa China, hii pia imesukuma mbele maendeleo kati ya China na nchi wanachama wa APEC. Tokea mwaka 1993, rais wa China kila mwaka huhudhuria mkutano usio rasmi wa viongozi wa APEC, ambapo hutoa mapendekezo na msimamo wa kikanuni wa China, hayo yamechangia mafanikio ya mkutano. Mwaka 2001, China ilifaulu kuendesha mkutano usio wa rasmi wa viongozi wa APEC huko Shanghai, China.

Shirika la biashara duniani WTO na China

Mwezi Aprili, 1994, mkutano wa mawaziri kuhusu Mkataba mkuu wa biashara forodhani uliofanyika huko Marrakech, Morocco uliamua kuanzisha rasmi Shirika la biashara duniani. Tarehe 1 Januari, 1995, Shirika la biashara duniani WTO lilianzishwa. Nia ya shirika hilo ni kusukuma mbele maendeleo ya uchumi na biashara ili kuinua kiwango cha maisha, kuhakikisha watu wengi wanapata ajira, kuhakikisha mapato na mahitaji halisi yanaongezeka; kutumia ipasavyo maliasili duniani, kupanua uzalishaji wa bidhaa na kazi ya huduma; kufikia makubaliano ya kunufaishana; kupunguza kwa kiasi kikubwa na kufuta ushuru forodha na kuondoa vikwazo vingine vya kibiashara. Nchi wanachama wa WTO zimefikia 144, na makao makuu yake yako Geneva.

Tokea mwaka 1986 China itoe ombi la kurudisha hadhi ya nchi iliyosaini mkataba mkuu wa biashara forodhani, China imefanya juhudi nyingi kubwa ili kujiunga tena na Shirika la biashara duniani WTO. Tokea mwezi Januari hadi Septemba, 2001, kikundi cha kazi ya China cha WTO kilifanya mkutano mara 4, na kukamilisha mazungumzo ya pande nyingi kuhusu China kujiunga na WTO, pia kupitisha nyaraka za sheria kuhusu China kujiunga na WTO. Tarehe 9 hadi 14 Novemba mwaka huo, mkutano wa 4 wa mawaziri wa WTO ulifanyika huko Doha, Qatar, waziri wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na nje wa China Bwana Shi Guangsheng aliongoza ujumbe kuhudhuria mkutano, ambapo China ilisaini makubalino ya kujiunga na WTO. Tarehe 19 hadi 20 mwaka huo, China ikiwa nchi mwanachama rasmi wa WTO ilihudhuria mkutano wa Baraza kuu la shirika la WTO.


1 2 3 4 5 6 7