4: Maingiliano na Nchi za Nje

Sera ya Kidiplomasia za China

China inatekeleza kithabiti sera ya kidiplomasia ya amani ya kujitawala na kujiamulia, lengo la kimsingi la sera hiyo ni kulinda uhuru, mamlaka na ukamilifu wa ardhi wa China, na kujenga mazingira mazuri ya kimataifa kwa ajili ya mageuzi na ufunguaji mlango na ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, kulinda amani ya dunia, na kusukuma mbele maendeleo ya pamoja. Mambo makubwa katika sera hiyo ni kama yafutayo:

Kufuata tangu mwanzo mpaka mwisho kanuni ya kujitawala na kujiamulia mambo, kutofungamana na nchi yoyote au kundi la nchi, kutounda kundi la kijeshi, kutoshiriki kwenye ushindani wa zana za kijeshi na kutofanya upanuzi wa kijeshi.

Kupinga umwamba, kulinda amani ya dunia, kutetea nchi kubwa au ndogo, nchi yenye nguvu au dhaifu, nchi maskini au tajiri zote ni nchi wanachama zenye usawa. Nchi na nchi zinapaswa kufanya mashauriano ya amani kwa kutatua migogoro kati yao, kutotumia nguvu za kijeshi au kuzitishia nchi nyingine kwa nguvu za kijeshi, na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa kisingizio chochote.

Kufanya juhudi za kuhimiza uanzishaji wa utaratibu mpya wa kisiasa na kiuchumi duniani. Kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani na kanuni nyingine zilizotambuliwa duniani kuhusu uhusiano wa kimataifa zingekuwa msingi wa kuanzisha utaratibu mpya wa kisiasa na kiuchumi duniani.

China inapenda kuanzisha na kuendeleza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano na nchi nyingine zote duniani kwenye msingi wa kanuni tano za kuheshimu mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi, kutoshambaliana, kutoingiliana mambo ya ndani, kuwa na usawa na kunufaishana na kuishi pamoja kwa amani.

Kutekeleza sera ya kuzifungulia mlango nchi za nje kwenye sekta zote, kuanzisha mawasiliano ya kibiashara, ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia na maingiliano ya kisayansi na kiutamaduni na kusukuma mbele usitawi kwa pamoja kwenye msingi wa kanuni za kuwa na usawa na kunufaishana.

Kujitahidi kushiriki katika shughuli za kidiplomasia za pande nyingi ni nguvu ya kithabiti kwa kulinda amani ya dunia na utulivu wa kikanda.

Katika zaidi ya miaka 50 iliyopita tangu kuzaliwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, China imekuwa na sera kamili za kidiplomasia zenye umaalum wa China. Katika siku za usoni, hali ya kuwepo kwa ncha nyingi na utandawazi wa uchumi duniani itaendelea, uhusiano wa kimataifa unarekebishwa kwa kina. Kutaka amani, kutafuta ushirikiano na kusukuma mbele maendeleo kumekuwa sauti ya pamoja ya wananchi wa nchi mbalimbali. Mambo ya kidiplomasia ya China pia yanakabiliwa na fursa na changamoto. China inapaswa kutumia fursa na kukabiliana na changamoto chini ya uongozi wa kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China, kufungua ukurasa mpya wa kazi ya kidiplomasia, kujenga mazingira mazuri zaidi ya amani ya kimataifa na kutoa mchango kwa juhudi za amani na maendeleo ya dunia.


1 2 3 4 5 6 7