4: Maingiliano na Nchi za Nje

Mawaziri wa mambo ya nje wa China wa awamu mbalimbali

Zhou Enlai

Zhou Enlai: Alikuwa waziri wa mambo ya nje wa China kuanzia mwaka 1949 hadi 1958.

Zhou Enlai alikuwa mwanamapinduzi, mwanasiasa, mtaalamu wa kijeshi na kidiplomasia wa China, pia alikuwa mmoja kati ya viongozi wakubwa wa Chama cha kikomunisti cha China na Jamhuri ya watu wa China, na mmoja kati ya waanzilishi wa Jeshi la ukombozi wa umma la China. Alizaliwa Huaian mkoani Jiangsu tarehe 5 Machi, 1898, alifariki dunia mwezi Januari, 1976.

Zhou Enlai aliwahi kutunga na kutekeleza sera nyingi za kidiplomasia za China. Mwaka 1954 alihudhuria mkutano wa Geneva. Mkutano huo ulitatua suala la Indo-China, na kuifanya jumuiya ya kimataifa itambue uhuru wa nchi tatu Vietnam (isipokuwa sehemu yake ya kusini), Laos na Cambodia. Zhou Enlai aliiwakilisha China kutetea kanuni za kuishi pamoja kwa amani ichukuliwe kuwa kanuni za uhusiano kati ya nchi na nchi. Mwaka 1955 kwenye mkutano wa Bandung uliofanyika nchini Indonesia, alitetea kuishi pamoja kwa amani, kupinga ukoloni, kutetea kutafuta maoni ya pamoja wakati wa kuweka kando migongano, na kufanya mashauriano kwa kauli moja. Aliwahi kufanya ziara katika nchi kumi kadhaa za Ulaya, Asia na Afrika, aliwahi kuwapokea viongozi na marafiki wengi kutoka nchi mbalimbali duniani, na kuongeza urafiki kati ya wananchi wa China na nchi mbalimbali duniani.

Chen Yi

Chen Yi: Alikuwa mmoja kati ya waanzilishi na viongozi wa Jeshi la ukombozi wa umma la China, ambaye pia ni mtaalamu wa kijeshi na jenerali mkuu wa Jamhuri ya watu wa China. Baada ya kuzaliwa kwa China mpya, aliwahi kuwa naibu waziri mkuu, waziri wa mambo ya nje na naibu mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi.

Kuanzia mwaka 1958 akiwa naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje, alifanya juhudi kubwa kutekeleza sera na fikra za kidiplomasia Mao Zedong na Zhou Enlai, kushiriki katika utungaji wa mikakati na sera za kidiplomasia za China mpya, kumsaidia Zhou Enlai kushiriki shughuli nyingi muhimu za kidiplomasia.

Ji Pengfei

Ji Pengfei: Alikuwa waziri wa mambo ya nje wa China toka mwaka 1972 hadi 1974.

Aliwahi kuwa balozi wa kwanza wa China nchini Ujerumani mashariki, naibu waziri wa mambo ya nje na waziri wa mambo ya nje. Baada ya mwaka 1979, alikuwa mkuu wa idara ya mawasiliano na nje ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, naibu waziri mkuu na katibu mkuu wa baraza la serikali. Alipokuwa mkurugenzi wa ofisi ya mambo ya Hong Kong na Makau na mjumbe mkurugenzi wa kamati ya utungaji wa mswada wa sheria ya kimsingi ya mikoa ya utawala maalum ya Hong Kong na Makau ya Jamhuri ya watu wa China, alitekeleza sera ya serikali ya China ya "nchi moja mifumo miwili" kwa kutatua kiamani masuala ya Hong Kong na Makau, na kuhudhuria sherehe ya kusainiwa kwa taarifa ya pamoja ya China na Uingereza kuhusu suala la Hong Kong.

Qiao Guanhua

Qiao Guanhua: Alikuwa waziri wa mambo ya nje wa China toka mwaka 1974 hadi 1976.

Alizaliwa huko Yancheng mkoani Jiangsu. Aliwahi kusoma nchini Ujerumani na alipata shahada ya tatu ya falsafa. Wakati wa kupambana na uvamizi wa Japan, alishughulikia kazi za habari na kuandika makala za maelezo kuhusu habari za kimataifa. Baada ya kuzaliwa kwa Jamhuri ya watu wa China, alikuwa naibu mkurugenzi wa kamati ya sera ya kidiplomasia katika wizara ya mambo ya nje ya China, msaidizi wa waziri wa mambo ya nje, na naibu waziri wa mambo ya nje. Katika shughuli zake za kawaida, alitunga mara kwa mara au kuandika nyaraka muhimu za mambo ya kidipolomasia.

Huang Hua

Huang Hua : Alikuwa waziri wa mambo ya nje wa China toka mwaka 1976 hadi 1982.

Huang Hua alikuwa mwakilishi wa kudumu wa kwanza wa China katika Umoja wa Mataifa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa tokea China irudishiwe kiti cha halali kwenye Umoja wa Mataifa. Alipokuwa waziri wa mambo ya nje aliwahi kuongoza ujumbe wa China kuhudhuria mkutano wa Baraza kuu la awamu za 29, 32, 33, 35 na 37 la Umoja wa Mataifa. Mwezi Agosti, 1978, hapa Beijing, Huang Hua na waziri wa mambo ya nje wa Japan walisaini "Mkataba wa amani na urafiki wa Jamhuri ya watu wa China na Japan". Mwaka 1978, aliendesha mazungumzo na mwakilishi wa Marekani kuhusu kuanzisha uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani, na mwaka 1982, Huang Hua na waziri wa mambo ya nje wa Marekani walisaini Taarifa ya tarehe 17, Agosti kuhusu Marekani kuiuzia Taiwan silaha. Hivi sasa bado anashika nyadhifa mbalimbali za jumuiya za China.

Wu Xueqian

Wu Xueqian : Alikuwa waziri wa mambo ya nje wa China toka mwaka 1982 hadi 1988.

Aliwahi kuwa naibu waziri mkuu wa China, mjumbe wa taifa na waziri wa mambo ya nje. Alipokuwa mjumbe wa taifa na waziri wa mambo ya nje aliwahi kufanya ziara katika nchi zaidi ya 50 kama vile, Korea ya kaskazini, Malaysia, Japan, Misri, Kenya, Zambia, Romania, Ufaransa, Ujerumani, Marekani, Canada, Argentina, na Brazil.

Qian Qichen

Qian Qichen : Alikuwa waziri wa mambo ya nje wa China toka mwaka 1988 hadi 1998.

Alizaliwa Mwezi Januari, 1928, huko Jiading, Shanghai. Toka mwaka 1972 hadi 1982, alikuwa balozi mdogo wa China nchini Urusi ya zamani, balozi wa China nchini Guinea, mkurugenzi wa idara ya habari katika wizara ya mambo ya nje ya China. Kuanzia mwaka 1988, alikuwa waziri wa mambo ya nje, katibu wa kamati ya chama na mjumbe wa taifa. Kuanzia mwaka 1993 alikuwa mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa China.

Tang Jiaxuan

Tang Jiaxuan: Alikuwa waziri wa mambo ya nje wa China toka mwaka 1998 hadi 2003.

Alizaliwa Mwezi Januari, 1938 huko Shanghai, maskani yake ni Zhengjiang mkoani Jiangsu. Toka mwaka 1970 hadi 1978, alikuwa ofisa katika shirikisho la urafiki wa watu wa China na nchi za nje na shirikisho la urafiki wa China na Japan. Alikuwa balozi mdogo na balozi wa China nchini Japan toka mwaka 1988 hadi 1999. Alikuwa msaidizi wa waziri wa mambo ya nje toka mwaka 1991 hadi 1993. Alikuwa naibu waziri wa mambo ya nje toka mwaka 1993 hadi 1998. Alikuwa waziri wa mambo ya nje mwaka 1998. Amekuwa mjumbe wa kitaifa kuanzia Mwezi Machi, 2003.

Li Zhaoxing

Li Zhaoxing : Amekuwa waziri wa mambo ya nje wa China kuanzia mwaka 2003 mpaka sasa.

Alizaliwa Mwezi Oktoba, 1940 mkoani Shangdong, alihitimu masomo katika chuo kikuu cha Beijing mwaka 1964. Aliwahi kufanya kazi katika ubalozi wa China nchini Kenya. Alikuwa naibu mkurugenzi na mkurugenzi wa idara ya habari katika wizara ya mambo ya nje na msemaji wa wizara hiyo toka mwaka 1985 hadi 1990. Alikuwa mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa toka mwaka 1993 hadi 1995. Alikuwa balozi wa China nchini Marekani toka mwaka 1998 hadi 2001. Alikuwa naibu waziri wa mambo ya nje toka mwaka 2001 hadi 2003. Mwezi Machi, 2003 alichaguliwa kuwa waziri wa mambo ya nje wa China.


1 2 3 4 5 6 7