11: Mikoa ya Xinjiang na Tibet

Xinjiang

Hali ya Xinjiang

Mkoa unaojiendesha wa kabila la wauigur wa Xingjian kwa ufupi unaitwa Xingjian. Uko katika sehemu ya kaskazini magharibi ya China na katikati ya sehemu ya bara ya Ulaya na Asia, ina eneo la kilomita za mraba zaidi ya milioni 1.66 na ni wa kwanza kwa ukubwa miongoni mwa mikoa ya China. Kwa upande wa magharibi na upande wa kaskazini, unapakana na nchi 8 zikiwa ni pamoja na Mongolia, Shirikisho la Russia, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Afghanistan, Pakistan na India, ambapo urefu wa mpaka umezidi kilomita 5,400. Xingjian ni mmoja wa mkoa wa China unaochukua nafasi ya kwanza kwa urefu mkubwa wa mpaka na wingi wa idadi ya forodha nchini China.

Mazingira ya Kijiografia

Xinjiang iko katika sehemu ya ndani ya Asia, kutoka upande wa kaskazini hadi upande wake wa kusini kuna milima ya Aertai, Tian na Kunlun pamoja na mabonde ya Zhungeer na Tulufan kati ya milima hiyo. Watu wamezoea kuiita sehemu ya kusini ya mlima wa Tian kuwa "Xinjiang ya Kusini", na sehemu ya kaskazini ya mlima wa Tian kuwa "Xinjiang ya Kaskazini" na kuita mabonde ya Hami na Tulufan "Xinjiang ya Mashariki". Miji na vijiji vya Xinjiang vyote viko pembezoni mwa mabonde mawili kama mkufu wa lulu.

Mkoani Xinjiang kuna mto Talimu, ambao ni wa kwanza kwa urefu kwenye sehemu ya ndani ya bara, pamoja na ziwa la Bositeng lenye maji baridi, ambalo ni la kwanza kwa ukubwa kwenye sehemu ya ndani ya bara na bonde la Tulufan, ambalo ni la kwanza kwa kuinama chini kabisa nchini China. Xinjiang iko kwenye sehemu yenye ukame na yenye tofauti kubwa sana kati ya hali joto ya mchana na usiku, sehemu ya Aletai ina rekodi kuwa na hali joto baridi kabisa, wakati sehemu ya Tulufan inakwenda kinyume chake kabisa nchini China.

Theluthi mbili za eneo la jangwa nchini China ziko mkoani Xingjian, ambayo eneo la jangwa la Takelamagan ni kilomita za mraba elfu 33, ni la kwanza kwa ukubwa nchini na ni jangwa la pili kwa ukubwa linalohamahama duniani. Jangwa la Guerbantonggute lililoko kwenye bonde la Zhungeer lina eneo la kilomita za mraba elfu 48, ambalo ni la pili kwa ukubwa hapa nchini. Katika majangwa ya nchini kuna rasilimali nyingi za mafuta ya asili ya petroli na gesi asili.

Milima yenye theluji na barafu mkoani Xingjian imekuwa chimbuko la maji ya mito. Wastani wa rasilimali wa mkazi wa Xingjian unachukua nafasi ya mbele nchini.

Ufuatiliaji wa Historia

Kabla ya miaka zaidi ya 2,000 iliyopita, Xinjiang ilikuwa moja ya sehemu ya umoja wa makabila mengi ya China. Mwaka 60 KK, enzi ya Han ilianzisha serikali kwenye eneo la magharibi, ambapo Xinjiang ilisimamiwa moja kwa moja na utawala wa enzi ya Han ya magharibi, na eneo lake lilikuwa pamoja ziwa la Baerkashi na sehemu ya Pamier ya hivi sasa. Katika muda wa miaka zaidi ya 1,000 hapa baadaye, sehemu ya Xinjiang imekuwa ikidumisha uhusiano wa kuwa himaya ya serikali kuu ya China, ambayo vitengo vya utawala vilivyowekwa na serikali kuu vimekuwa vikisimamia shughuli za Xinjiang.

Katika enzi ya Qing, miaka zaidi ya 300 iliyopita, serikali kuu ilimweka jemedari wa Yili kwenye mji wa Huiyuan, sehemu ya Yili, Xinjiang, ambaye alitawala eneo lote la Xinjiang. Mwaka 1884, ulianzishwa mkoa wa Xinjiang, ambapo uhusiano kati yake na mikoa mingine ya China uliimarishwa zaidi.

Mwezi Septemba mwaka 1949, Xinjiang ilipata uhuru kwa njia ya amani. Tarehe 1 mwezi Oktoba mwaka huo huo ilianzishwa Jamhuri ya Watu wa China, ni kama mikoa mingine ya China Xinjiang ilikuwa mkoa unaojiendesha kikabila nchini China.

Kituo cha Nishati

Xinjiang ina rasilimali tele, kiasi cha makaa ya mawe na gesi ya asili ni theluthi moja ya idadi ya jumla vitu hivyo vilivyogunduliwa, gesi ya asili pia ni nyingi na kuchukua nafasi ya kwanza katika sehemu ya kaskazini magharibi ya China. Inakadiriwa kuwa kwenye eneo lenye mafuta na gesi la kilomita za mraba elfu 740, kuna mafuta ya asili ya petroli tani bilioni 20.8 na mita za ujazo trilioni 1 ya gesi ya asili zikiwa ni kiasi cha 30% ya jumla ya rasilimali za mafuta na gesi ya asili zilizoko kwenye nchi kavu na kusifiwa na wataalam wa China na wa nchi za nje kuwa ni "bahari yenye matumaini" ya sekta ya usafishaji wa mafuta ya petroli nchini. Mradi wa kupeleka gesi ya asili ya sehemu ya magharibi kwa sehemu ya mashariki ya China, ambao ujenzi wake utakamilika mwezi Oktoba mwaka huu, na utasafirisha kiasi kikubwa cha gesi kwenye sehemu ya mashariki ya China ikiwemo mji wa Shanghai na sehemu ya pembezoni mwake.

Rasilimali ya makaa ya mawe ya Xinjiang ni kiasi cha tani elfu 20, kiasi hicho ni kama 40% ya jumla ya raslimali ya makaa ya mawe nchini ikichukua nafasi ya kwanza kwa wingi wa makaa ya mawe hapa nchini.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13