11: Mikoa ya Xinjiang na Tibet

Tibet

Hali ya Tibet

Mkoa wa Tibet ni moja ya mikoa mitano inayojiendesha yenyewe nchini China, kwa ufupi mkoa huo unaitwa kuwa Tibet. Tibet iko katika sehemu ya kusini magharibi ya China ikipakana na nchi za Myanmar, India na Bhutan na Nepal kwenye upande wake wa kusini na upande wa magharibi, urefu wa mpaka unakaribia kilomita 4,000. Eneo la Tibet ni kiasi cha kilomita za mraba milioni 1.22 likichukua 12.8% ya eneo la China.

Wastani wa urefu wa mwinuko mkoani Tibet ni zaidi ya mita 4,000, hivyo inajulikana kwa "Paa la Dunia". Idadi ya wakazi wa Tibet ni zaidi ya milioni 2.6, kati yake idadi ya watu wa kabila la watibet ni milioni 2.5 ikichukua 96% ya jumla ya idadi ya watu wa Tibet. Tibet ni mkoa wenye idadi ndogo kabisa ya watu nchini China, na pia ni mkoa wa kwanza wenye idadi ndogo ya wakazi kwenye eneo la kilomita za mraba moja, ambalo ni pungufu ya watu wawili kwenye eneo la kilomita moja ya mraba.

Hali ya Kijiografia

Uwanda wa juu wa Qingzang una umaalumu pekee wa kimaumbile, ambao unachukua nafasi muhimu katika nyanda za juu na milima mikubwa, na kujulikana kwa "ncha ya tatu ya dunia".

Sababu za kuitwa "ncha ya tatu ya dunia" kunatokana na kuinuka juu kwake na hewa baridi inayohusika. Wastani wa mwinuko wake ni mita zaidi ya 4,000 juu ya usawa wa bahari pamoja na milima mikubwa iliyoko katika pembezoni mwa uwanja wa juu.

Historia na Hali Yake ya Hivi Sasa

Kabla ya kuzaliwa Yesu Kristu, mababu jadi wa watibet walioishi kwenye uwanda wa juu wa Qingzang walikuwa na uhusiano na watu wa kabila la wahan walioishi sehemu ya ndani ya China. Baada ya kupita miaka mingi, watu wa makabila mbalimbali walioishi kwenye uwanda wa juu waliungana na kuwa wa kabila la watibet.

Hali ya vurugu na ya mfarakano iliyoendelea kwa miaka zaidi ya 300 ilimalizika mwanzoni mwa karne ya 7. Shujaa wa watibet Songzanganbu alianzisha rasmi enzi ya Turufan na kufanya Lahsa kuwa mji mkuu wake, ambapo walijifunza mafanikio ya teknolojia ya kisasa ya uzalishaji mali na siasa na utamaduni wa enzi ya Tang na kudumisha uhusiano wa kirafiki na enzi ya Tang katika mambo ya siasa, uchumi na utamaduni.

Katikati ya karne ya 13 sehemu ya Tibet iliingizwa katika nchi ya China na ilitawaliwa na serikali kuu pamoja na kuwepo kwa mabadiliko ya enzi kadhaa.

Baada ya kuanzishwa enzi ya Qing utawala kwenye sehemu ya Tibet uliimarishwa zaidi na kuwa wa kisheria na kiutaratibu.

Baada ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1949, serikali kuu iliamua kutekeleza sera ya kuikomboa Tibet kwa njia ya amani kutokana na historia na hali halisi ya huko. Serikali kuu ya umma ikifuata matarajio la watu wa Tibet ilifanya mageuzi ya demokrasia na kuvunja utaratibu wa kimwinyi katika Tibet, tokea hapo watumwa wa huko walipata uhuru na kutouzwa, kubadilishwa au kuwa mali ya matajiri ya kulipia madeni yao. Mkoa unaojiendesha wa Tibet ulianzishwa rasmi mwezi Septemba mwaka 1965.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13