11: Mikoa ya Xinjiang na Tibet

Rasilimali za Utalii za Xinjiang

Ziwa la Kanasi

Ziwa la Kanasi liko katika wilaya ya Buerjin iliyoko katika sehemu ya kaskazini yenye umbali wa kilomita 150 kutoka mji mkuu wa wilaya. Ziwa hilo liko ndani ya msitu mnene kwenye sehemu ya juu ya mlima likiwa na urefu wa mita 1374 juu ya usawa wa bahari, eneo la ziwa hilo ni kilomita za mraba 45.73 na sehemu yenye maji mengi zaidi ina kina cha mita 188.5.

Pembezoni mwa ziwa la Kanasi ni milima mirefu yenye barafu na theluji, mandhari yake ya asili inapendeza sana. Sehemu hiyo ni ya pekee nchini China yenye wanyama na mimea ya sehemu ya Siberia ya Kusini vikiwa na miti aina karibu 800 ikiwemo miti adimu ya spruce, fir na Korean pine, aina 39 za wanyama, aina 117 za ndege, wanyama wanaotambaa na kuweza kuishi ndani ya maji aina 4, aina 7 za samaki na wadudu aina zaidi ya 300, ambazo aina nyingi zake ziko katika sehemu hiyo tu. Sehemu hiyo ina mandhari nzuri ya mbuga yenye misitu kati yake, maziwa mengi na yenye thamani kubwa ya utalii, hifadhi ya mazingira ya asili, utafiti wa sayansi, historia na utamaduni.

Mji wa Kale wa Loulan

Mji wa kale wa Loulan uko katika sehemu ya kaskazini magharibi ya Luobubo, kusini mwa Xinjiang, ambao ulikuwa mji muhimu sana kwenye njia ijulikanayo kwa "njia ya hariri" hapo zamani. Hivi sasa mji huo umezungukwa na jangwa na chumvi iliyoganda imara, sehemu hiyo imekuwa pori lenye hatari na kutoonekana watu.

Kutokana na vitabu vya historia, mnamo karne ya 2 kabla ya Kristo, Loulan ilikuwa moja ya sehemu iliyoendelea sana kwenye sehemu ya magharibi ya China. Kitu kinachoshangaza ni kwamba dola hilo, ambalo jina lake lilivuma sana, lilitoweka ghafla baada ya kustawi kwa miaka zaidi ya mia 5 au 6. Mji wa kale wa Loulan ulitoweka namna gani? Toka muda mrefu uliopita, suala hilo jambo hilo lilikuwa suala linalofuatiliwa na watafiti wa mambo ya kale na wanasayansi. Loulan pamekuwa mahali penye siri na ajabu panapovutia watu wanaotaka kuvumbua siri ya maumbile ya asili duniani.

Kutokana na uchunguzi uliofanywa kuhusu mji wa kale wa Loulan, mji huo ulitoweka kwa kufunikwa na jangwa kutokana na chanzo cha kimaumbile na shughuli za binadamu ambazo zilifanya maji ya mto kutiririka kwa kubadilisha njia yake. Kutokana na uchunguzi kuwa mji wa kale wa Loulan ulikuwa na eneo la mita za mraba elfu 120, ambao kuta za mji huo zilitengenezwa kwa udongo, matete (bulrush) na vijiti vya miti. Mto mmoja karibu ulipitia katikati ya mji huo kutoka upande wa kaskazini magharibi hadi upande wa kusini mashariki, lakini vilivyobaki hadi hivi sasa ni mnara wa dini ya kibudha pamoja na majengo yaliyoko karibu na mnara huo. Karibu na mji huo kuna mabaki ya mnara wa kupasha habari wakati wa dharura, maghala ya nafaka na makaburi. Ndani ya makaburi ya mji wa Loulan ilifukuliwa maiti kavu ya "mrenbo wa Loulan" ya kabla ya miaka 3,800 iliyopita. Sasa ndani ya mji wa kale wa Loulan bado kuna mabaki ya vipande vya vyungu vya zamani, maturubai ya sufu, nguo zilizochanika na kuoza za hariri pamoja na pesa za shaba na silaha za kale

Pango lenye Sanamu za Kibudha

Kwenye "njia ya hariri" ndefu ya kuelekea Xinjiang kuna mabaki ya majengo ya ngome yanayojulikana duniani, malango ya njia, hekalu la pango la mawe, nyumba za wageni, makaburi na minara ya kupasha habari wakati usalama unapotishiwa.

Pango lenye sanamu za kibudhaa elfu moja lililoko Kezier na pango la sanamu za kibudha elfu moja lililoko Baizikelike ni mapango maarufu zaidi kutokana na sanamu na mapicha yaliyochongwa na kuchorwa kwenye kuta za pango la mawe ambazo zimeunganisha utamaduni wa China, India na uajemi na kuonesha hali ya uzalishaji mali na maisha ya wakati wa makabila mbalimbali.

Mapango hayo yalitobolwa toka karne ya 6 hadi karne ya 14 kaskazini mashariki ya mji wa Turufan ingawa baadhi ya sanamu na mapicha kwenye kuta za mapango yameharibiwa, lakini eneo linalohifadhiwa bado limefikia mita za mraba zaidi ya 1,200, ambapo panatambuliwa kuwa ni mahali panapohifadhiwa vizuri zaidi penye sanaa za dini ya kibudha duniani.

Tulufan

Kwenye bonde linaloinama chini sana, sehemu ya kati ya Xinjiang kuna mahali panapojulikana kama "ardhi ya moto", sehemu hiyo inaitwa kwa jina na Tulufan. Kutokana na hali maalumu ya kijiografia, Tulufan ina maji mengi chini ya ardhi, hivyo ni mahali pazuri kwa ukuaji wa mizabibu, matikiti maji na matunda mengine. Kutokana na uhaba wa mvua, matunda yanayozalishwa huko ni matamu zaidi, kuna watalii wengi wanaokwenda huko kwa lengo la kula matunda.

Kashi

Jina kamili la Kashi ni "Kashigeer", sehemu hiyo inasifiwa kuwa ni "lulu iliyoko kwenye njia ya hariri" na ni mji wa kale wenye utamaduni wa miaka mingi.

Kashi ni sehemu yenye maji na mimea kwenye upande wa magharibi wa bonde la Talimu tangu zamani za kale.

Sehemu ya Kashi ina raslimali kubwa ya utalii kutokana na mandhari yake nzuri, jangwa, milima yenye barafu na theluji pamoja na milima mizuri.

Kashi inavutia sana watalii kutokana na utamaduni na majengo maalumu wa kiurgur, hata watu wamesema kuwa "mtu asiyefika Kashi haonekani kama amefika Xinjiang".

Hetian

Hetian ni moja ya nchi ya kale yenye ustaarabu kwenye sehemu ya magharibi. Hetian iko kwenye sehemu ya ndani ya mabara ya Asia na Ulaya na ilichukua nafasi muhimu kwenye njia ya hariri ya zamani, wakazi wa makabila mbalimbali wanaishi pamoja huko na kuleta mchanganyiko wa utamaduni wa mashariki na magharibi.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13