11: Mikoa ya Xinjiang na Tibet

Makabila ya Xinjiang

Kabila la Wauigur

Kabila la wauigur ni moja ya makabila yaliyokuweko toka zamani za kale, "uigur" ni jina wanalojiita, ambalo maana yake ni "umoja" au muungano". Kabila la wauigur, ambalo idadi ya watu inazidi milioni 7, ni kubwa kwenye sehemu ya Xinjiang,. Kabila hilo la watu lina lugha na maandishi yake.

Mavazi ya jadi ya wauigur ni kuwa wanaume kwa wanawake na wazee kwa watoto wote wanapenda kuvaa makofia ya pembe nne na yenye nakshi za kutariziwa. Wanaume wanapenda kuvaa kanzu na shati ndani yake. Wanawake wanapenda kuvaa gauni na vizibau vyeusi nje, kuvaa hereni, bangili, pete na mikufu, wasichana wanapenda sana kusuka nywele zenye mikia mingi. Wakazi wa mijini hivi sasa wanavaa mavazi ya kisasa.

Watu wa kabila la wauigur wana adabu kubwa, wanapoona wazee au marafiki, wanazoea kuweka mikono yao ya kulia kwenye katikati ya kifua na kuinama kwa mbele huku wanawasalimia.

Watu wa Kabila la Wakazakh

Xinjiang ina idadi ya wakazakh kiasi cha milioni 1.2, wengi wao wanaishi kwenye jimbo linalojiendesha la kabila la wakazakh, sehemu ya kaskazini ya Xinjiang. Kabila la wakazakh lina lugha na maandishi yake yenyewe.

Wengi wa watu wa kabila hilo ni wafugaji, ambao wanahamahama kwa kufuatana na hali ya malisho katika majira mbalimbali ya mwaka isipokuwa baadhi ya wachache alioshughulikia uzalishaji wa mazao ya kilimo na kukaa katika nyumba za kudumu.

Kwenye sehemu za malisho, wafugaji wanaishi katika nyumba za mviringo zilizotengenezwa kwa nguo ya sufu, ambazo zinaweza kuondolewa na kuhamishwa isipokuwa katika majira ya siku za baridi, ambayo wanaishi ndani ya nyumba zilizojengwa kwa udongo zenye mapaa ya bapa. Watu wa kabila la wakazakh wanapenda kula vyakula viliivyotengenezwa kwa maziwa ya ng'ombe, kondoo na mbuzi na kunywa maziwa pamoja na chai yenye maziwa. Kwenye sehemu za malisho wafugaji wanapenda kula nyama na matumbo ya farasi.

Watu wa kabila la wakazakh wanapenda kuwakaribisha wageni kwa ukarimu mkubwa na kuchinja kondoo.

Wanaume kwa wanawake wa kabila la wakazakh wanajua sana kupanda farasi. Vijana wanapenda kupigana mieleka na mchezo wa kushindania kondoo wakipanda kwenye farasi.

Kabila la wa Tadzhik

Idadi ya watu wa kabila la watadzhik mkoani Xinjiang imefikia zaidi ya elfu 36, na wengi wao wanaishi kwenye wila inayojiendesha ya Tadzhik. Watu wengi wa kabila hilo ni wafugaji na pia wanafanya shughuli za kilimo. Tangu karne nyingi zilizopita walikuwa wamejenga makazi yao kwenye mabonde yenye urefu wa mita kiasi cha 3,000 juu ya usawa wa bahari, wanapanda mbegu za mazao yanayovumilia baridi katika majira ya Spring, kisha wanaswaga mifugo yao kwenye malisho yenye majani yaliyoko kwenye milima, ikifika majira ya kupukutika majani wanarejea vijijini kuvuna mazao waliyopanda na kukaa nyumbani katika siku za baridi kali, wanaishi hivyo mwaka nenda na mwaka rudi. Mwanaume anapenda kuvaa kanzu ndefu isiyo na ukosi na kufunga mkanda kiunoni, katika siku za baridi anavaa koti refu na kofia ndefu iliyoshonwa kwa ngozi ya kondoo. Wanapenda kula samli na vyakula vilivyotengenezwa kwa maziwa.

Watu wa kabila la watadzhik wanayo lugha na maandishi yao. Wanapocheza ngoma huiga mwewe anavyoruka. Mwewe ni alama ya ushujaa, hivyo watu wa kabila hilo wanaita kabila lao ni la mwewe.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13