11: Mikoa ya Xinjiang na Tibet

Makabila ya Tibet

Hali ya Makabila

Mkoa unaojiendesha wa Tibet ni sehemu wanayokaa kwa wingi watu wa kabila la watibet nchini China wakichukua 45% ya jumla ya idadi ya wakazi wa huko. Mbali na kabila la watibet, kuna makabila mengine ya wameba, wageba, wahan, wadeng na washaerba.

Kabila la Watibet

Kabila la watibet ni lenye idadi kubwa ya watu kwenye sehemu ya Tibet. Watibet wanashughulikia zaidi kazi za kilimo na ufugaji, wakati wakazi wa mijini wanashughulikia kazi ndogo ndogo za ufundi, uzalishaji bidhaa viwandani na biashara.

Watibet ni waumini wa dini ya kibudhaa ya kitibet. Watu wa kabila hilo ni wachangamfu na ni hodari sana kwa uwindaji na uchezaji ngoma. Watibet wanapenda kuvaa mashati yenye mikono mirefu; wanaume wanavaa kanzu kubwa nje, wanawake wanavaa kanzu isiyo na mikono na kufunga mkanda kiunoni, na wanawake walioolewa wanapenda kuvaa vitambaa vyenye rangi mbalimbali kama za upinde wa mvua. Wanaume kwa wanawake wanapenda kufuga nywele ndefu na kusuka mikia ya nywele na kupenda kuvaa mapambo ya hereni, bangili na pete. Chakula kikuu cha watu watibet ni unga wa mseto wa shayiri ya uwanda wa juu (highland barley) na choroko na kupenda kunywa chai ya samli na pombe na kula nyama za ng'ombe na kondoo.

Kabila la wamenba

Kabila la wamenba ni kabila la kale kwenye Uwanda wa juu wa Tibet, watu wengi wa kabila hilo wanaishi katika sehemu ya kusini ya Mkoa unaojiendesha wa Tibet. Wamenba wanategemea kazi ya kilimo na ufugaji, uwindaji na kazi ndogo ndogo za mikono. Wamemba wote wanapenda kunywa pombe na kuvuta tumbaku. Wengi wanaamini dini ya kibudha ya kitibet.

Kabila la waloba

Waloba wengi wameenea katika sehemu ya kusini mashariki ya Mkoa unaojiendesha wa Tibet, waloba wanafanya shughuli za kilimo na kupenda kusuka vyombo vya mianzi.

Nguo za waloba wanaume na wanawake ni zenye mtindo maalum wa kabila hilo. Waloba wanapenda kula chakula cha mahindi, pia wanakula wali na chakula cha unga wa ngano.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13