WHO latoa mwito wa kueneza matumizi binafsi ya vipimo vya Ukimwi
Wiki hii ulimwengu umeadhimisha siku ya Ukimwi duniani tarehe 1 Desemba huku Shirika la Afya Duniani WHO likitoa mwongozo mpya wa kueneza matumizi binafsi ya vipimo vya UKIMWI, na kupanua upimaji wa virusi hivyo na matibabu ya kupambana na virusi vya UKIMWI.
WHO imesema, hivi sasa zaidi ya asilimia 40 ya watu walioambukizwa na virusi vya Ukimwi hawajui hali yao, hivyo upungufu wa vipimo vya virusi hivyo umekuwa tatizo kuu katika tiba ya ugonjwa huo.
Takwimu zilizotolewa na kituo cha udhibiti wa magonjwa cha China zinaonesha kuwa, hadi mwezi Septemba mwaka huu, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi na wagonjwa wa Ukimwi nchini China imefikia laki 6.54, na zaidi ya watu laki 2 walifariki kutokana na ugonjwa huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |