UNHCR lawarejesha wakimbizi elfu 35 wa Somalia kutoka Kenya
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema, limewasaidia wakimbizi zaidi ya elfu 35 wa Somalia kurudi nyumbani tangu kazi ya kuwarudisha wakimbizi hao ianze miaka miwili iliyopita.
Shirika hilo limesema, wakimbizi 327 walisaidiwa kurudi kwa hiari mjini Mogadishu kati ya Novemba 1 hadi 15.
Kenya inashirikiana na UNHCR kuwarudisha wakimbizi laki 3 wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab, baada ya nchi hiyo kutangaza kufunga kambi hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |