Rwanda yafungua uchunguzi dhidi ya maofisa 20 wa Ufaransa kuhusiana na mauaji ya halaiki
Rwanda imefungua uchunguzi wa jinai kuhusu ushiriki wa maofisa 20 wa jeshi la Ufaransa kwenye mauaji ya halaiki ya Rwanda yaliyotokea mwaka 1994, baadhi ya maofisa hao wanaweza kufikishwa mahakamani kama ikigundulika kuwa wana kesi ya kujibu.
Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na mwendesha mashtaka wa Rwanda Bw Richard Muhumbuza imesema, serikali ya Rwanda imefungua rasmi uchunguzi dhidi yao, ambao kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa, wanatakiwa kutoa maelezo kuhusu tuhuma dhidi yao ili serikali iweze kufanya uamuzi kama watashtakiwa au la.
Mwezi Oktoba kamati ya taifa ya kupambana na mauaji ya halaiki ya Rwanda ilitoa orodha ya majina ya maofisa 22 waandamizi wa jeshi la Ufaransa wanaotuhumiwa kusaidia upangaji wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |