Ngono imekuwa njia kuu zaidi ya maambukizi ya UKIMWI
Nalo shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema, maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi VVU kati ya vijana kwa mwaka yanaweza kuongezeka kutoka laki 2.5 ya mwaka 2015 hadi laki 4 ya mwaka 2030, kama mchakato wa uhamasishaji kwa vijana utakwama. Shirika hilo limesema, UKIMWI bado ni chanzo kikuu cha vifo kwa vijana, ambao umesababisha vifo vya vijana elfu 41 wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 19 mwaka 2015.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |