Mahakama Korea Kusini yamwondoa mamlakani rais Park Geun-hye
Mahakama nchini Korea Kusini imemwondoa mamlakani rais wa nchi hiyo Park Geun-hye.
Awali bunge nchini humo lilikuwa limepitisha hoja ya kumwondoa Rais huyo kutokana na tuhuma za ufisadi.
Majaji wote wa mahakama ya juu wameunga mkono uamuzi wa kuondolewa kwa Park.
Park anakuwa rais wa kwanza nchini humo kuondolewa mamlakani.
Amehusishwa na ufisadi pamoja na rafiki yake wa karibu
Choi Soon-sil.
Sasa hana kinga yoyote kama rais na huenda akafunguliwa mashtaka.
Kumekuwa na vurugu nje ya mahakama wafuasi wa Park wakikabiliana na polisi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |